Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Masumbuko alizaliwa kijijini na kulelewa na Mama yake tu baada ya Baba yake kumtelekeza akiwa na Umri wa miaka 2.
Mama yake alifanya kila aina ya KAZI, kupika pombe za asili (gongo), kupalilia kama kibarua, na kuuza mboga mboga.
Mama yake alifanya kila namna ili mwanae asilale njaa.
Mama Masumbuko aliamini katika elimu kama urithi na ukombozi kwa mwanae japokuwa hata yeye hakupata bahati ya kusoma.
Hivyo alimwandikisha shule mapema na kumpambania asome kwa bidii huku akifanya kila awezalo kumtimizia mahitaji yake ya msingi ili asikwame kimasomo.
Wakati wa likizo au wikiendi Masumbuko, “NO TUTION”. Huungana na Mama yake kwenda kufanya vibarua kwenye mashamba ya kahawa ili aweze kupata Mia Mbili Mia tatu Kwa ajili ya mahitaji ya shule ikifunguliwa.
Masumbuko ‘Ndoto’ ya elimu ikamwiita akaitika. Shuleni akawa anapambana kusoma kwa bidii.Pengine ni Kwa sababu ya shida za nyumbani LAKINI pia kwa ajili kumsaidia Mama yake.
Masumbuko alikula kiapo cha kutoboa, “I will not sleep until I make Mama Proud”.
Masumbuko akirudi nyumbani kutoka shuleni, Mama yake jioni humwambia soma Mwanangu kwa bidii.
Nyumba Yao ya nyasi na Udongo haikuwa na umeme wala Mwanga wa ‘Solar’. Alitumia Kibatari cha mafuta ya taa kujisomea au siku zingine kuchoma tairi (Mpira) ili kujisomea. Yaani, alijitahidi kufanya, “Homework” huku macho yanamuwasha.
Masumbuko alipomaliza shule ya msingi, Mungu si Athumani alitoboa kwenda Sekondari, LAKINI ada ikawa kimbembe.
Mama yake alirudi kuwalilia Kaka zake (wajomba zake Masumbuko). Wapo waliotaka kumsaidia na wapo pia waliomkejeli!!
‘Kamtafute Baba yake?’
‘Yaani Wewe Mwanamke Umezalishwa Kwa Starehe zako uje utusumbue?’
Wahenga walisema, “Inahitaji Kijiji kumkuza mtoto”. Wasamaria wema kijijini wakajichanga na kisha Masumbuko akapata fedha kidogo ya kuanza safari yake ya Sekondari.
Kwa kuwa alijua Hali ya nyumbani ikoje, shuleni alishika jambo moja Tu, “Kusoma”.
Alipambana akafaulu kwenda kidato cha tano. Mama yake akauza kipande kidogo cha aridhi alichorithishwa na Baba yake ili kumsaidia mwanae.
Masumbuko alipangiwa shule ya mbali huko Nyamagana, hivyo ilibidi aende bweni.
Shuleni ni Yeye na Kitabu, Likizo ni Yeye na Kibarua.
Mwamba akapambana akatoboa kidato cha sita. NDOTO yake ikakaribia kutimia. Kwa kuwa alitoka familia duni, yeye akasema Bora nisome ualimu ili nipate ajira mapema.
Akachaguliwa shahada ya Ualimu, Jiografia na Biolojia Chuo Kikuu Mlimani-DUCE.
Bahati nzuri alipata mkopo kwa hiyo hakukuwa na mahitaji makubwa zaidi ya nauli na matumizi kidogo ya kuanzia.
Kwa kuwa ameshakuwa mkubwa, hakutaka tena kumsumbua Mama yake.
Jamaa, aliangia mzigoni kufanya kazi ya saidia fundi, alikoroga zege na kupandisha matofali ili kupata nauli ya kuripoti chuo.
Siku hazigandi, Masumbuko alihitimu shahada yake vizuri. Mama yake alifurahi Sana Kwa sababu alijua fika hapo ndiyo mwisho wa matatizo Yao.
Hata Wajomba zake waliogoma kumsaidia walianza kumtafuta.
….Wajomba zake walianza kumtafuta na kumpigia simu ili kumjulia Hali. Si unajua Ngoma umekaribia kuiva alafu pia…..”Mjomba ni Mama
“
Walianza kujisafisha, “Mjomba wetu Sisi hatukuchukii bana Mama yako ndiyo alikuwa na shida
Masumbuko aliitikia tu, LAKINI kila akikumbuka na alivyoambatana na Mama yake kwenda Kwa Wajomba kuomba msaada ya Karo ya shule na waliambulia matusi….”Machozi yanamtoka”.
But, Ndiyo maisha na Walimwengu.
Masumbuko amesha-graduate kilichobaki SASA ni kupambana.
“Elimu ni Ufunguo wa Maisha”, kilichobaki SASA ni kutekenya kila kufuli la maisha mpaka lifunguke.
Masumbuko alianza ku-apply kila post ualimu inapotangazwa LAKINI majibu hakubahatika kuchaguliwa Kwa sababu, “Graduates” ni wengi na wanaajiri Kwanza wale wa miaka ya nyuma.
Masumbuko anasugua kichwa, nifanyaje SASA hapa mjini maana natakiwa kulipa Kodi na kijijini inabidi tena nimtumie ‘Maza’ hela kidogo.
Si unajua tena uzee ushaingia hawezi tena kukimbizana na vibarua kama zamani.
Miaka 2 sasa Masumbuko hana ajira. Anapambana kujishughulisha na shughuli ndogo ndogo huku akiwa bado na “TUMAINI juu ya NDOTO yake”.
Kila akitaka kukata tamaa, anakumbuka kiapo, “I will not sleep until…..”.
Umekula kiapo cha KUTOBOA?
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.