Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Majadiliano ya “Tumaini”, yaliyoandaliwa chini ya mwamvuli wa Kenya, kati ya serikali ya Sudani Kusini na makundi ya upinzani ambayo hayajatia saini makubaliano ya amani ya 2018, yamesitishwa. Sababu ni kutokubaliana kati ya pande tofauti

Nchini Kenya, mazungumzo ya amani ya “Tumaini” yamesitishwa tena. Yanafanyika jijini Nairobi na kuhusisha serikali ya Sudani Kusini na makundi yenye silaha ambayo hayajatia saini makubaliano ya amani ya mwaka 2018, kwa upatanishi wa mamlaka ya Kenya.
Ujumbe wa serikali ya Sudani Kusini unasema lazima urudi Juba kwa mashauriano. Hakuna jambo lisilo la kawaida, kulingana na upatanishi wa Kenya, ambao unahakikisha kwamba “maendeleo makubwa yamepatikana”.
Suala lingine, kwa upande wa makundi yenye silaha na vyama vya upinzani. Lual Dau, msemaji wa Muungano wa Vyama vya Upinzani vya Sudani Kusini, anachukulia majadiliano hayo kuwa katika mkwamo.
Pande mbalimbali zilikuwa zimekubaliana kuhusu masuala manne wanayopaswa kujadili: uhusiano kati ya mkataba unaojadiliwa kwa sasa na ule uliotiwa saini mwaka wa 2018 (je maandishi mapya yatakuwa kiambatisho rahisi au yatachukua nafasi ya makubaliano ya awali ya amani?), uanzishwaji wa taratibu za amani, kugawana majukumu, na hatimaye kalenda ya chaguzi zijazo (kwani Uchaguzi Mkuu wa Desemba umefutwa).
Lakini ujumbe wa serikali umepuuzilia mbali ajenda hii, kulingana na upinzani. “Baadhi ya wadau wanaharibu kila kitu kwa sababu wamejishughulisha sana na miundo yao ya kisiasa,” analaumu Edmund Yakani, mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Maendeleo na Uwezeshaji. Anatoa wito wa kuwajibika zaidi. Majadiliano yanapaswa kuanza tena mapema mwezi Januari.
Baada ya miezi kadhaa ya usumbufu, mazungumzo haya yalianza tena mwanzoni mwa mwezi Desemba, kufuatia ziara ya Rais wa Kenya William Ruto mjini Juba. Walitarajiwa kufikia makubaliano kabla ya Krismasi.
Sudani Kusini inatatizika kujikwamua kutokana na vita vya kikatili vya wenyewe kwa wenyewe kuanzia mwaka 2013 hadi 2018 kati ya vikosi vinavyomtii Salva Kiir, rais wa sasa wa nchi hiyo, na makamu wake wa sasa, Riek Machar. Vita ambavyo viliua takriban watu 400,000 na kuwalazimu mamilioni kuhama makazi yao.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.