Bao La Asubui-17-12-2024

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Kila siku unapoamka ni lazima uamue; wewe uiendeshe SIKU yako au siku IKUENDESHE wewe…

Haya ni maamuzi muhimu kwa sababu utakapoanza siku tu…

Utaanza kukutana na vitu vya KUKUUDHI…

Au KUKUKATISHA TAMAA.

Kwa uzoefu wangu, zile siku ambazo inatakiwa MAMBO MUHIMU yatokee kwenye maisha yako…

Ndio utaanza kukutana na “visanga” mapema sana.

Kuna habari zingine utatumiwa kwenye meseji/kupigiwa simu.

Kuna zingine utazisoma kwenye vyombo vya habari.

Au kuzishuhudia kwa macho.

Hata leo, kuna sababu nyingi za kukufanya UKATE TAMAA.

Au UUMIE.

Au URUDI NYUMA.

Uamuzi ni wako.

Ukiruhusu MANENO ya wengine yakuendeshe…

Na WAAMUE FURAHA yako, basi hautafika mbali.

Leo, DHAMIRIA kuwa:

Bila kujali nini kitatokea kwenye maisha yako…

Utaambiwa au utakisikia, USIKUBALI kikuendeshe.

Focus on Your Goals!

Kama umeipenda makala hii…

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment