Mwanamke ana uwezo mkubwa ni mjasiria mali.


Mwaka wa 2006 nikiwa Imani Radio kitale, niliulizwa swali la bila kutarajia ghafla na mtangazaji mweenzangu, swali lilikua unamzungumziaje mwanamke? Na unanini cha kumwambia mama yako?…. Kwa kuwa siku hiyo ilikua siku ya wanawake duniani. Majibu yangu yalikua kama yakuropoka lakini baadaye yakanipa ujumbe wa wimbo.

Nilijibu mwanamke ana uwezo wa Kiungu, ndio maana biblia imemtaja kama msaidizi, na neno msaidizi limejitokeza mara mbili tu kwa biblia, moja ikimtaja Eva kama msaidizi kwa Adamu na pili ikimtaja Roho Mtakatifu kama msaidizi kwa kanisa.

Ndio maana majukumu ya Roho mtakatifu ni kukumbusha, kuona ya mbeleni kabla hayajatokea, kusaidia udhaifu wetu, kutuombea, kututakasa, kutukamilisha, ….nk. Ambayo ukiyaangalia kwa undani hayapishani sana na majukumu ya mwanamke kwa mumewe.

Pia baadhi ya tabia za Roho mtakatifu ni mvumilivu, mpole, hulia aba, wivu kiasi cha kuugua, anapenda kusifiwa, ana huruma, ….nk ambazo pia mwanamke anazo.
Sasa kumbe hawa wanawake si viumbe dhaifu kama wengi tusemavyo, na ndio maana biblia haikuwahesabu kama watu si kwa sababu ya UDHAIFU WAO BALI KWA SABABU YA MAJUKUMU YAO WAO WAKO LEVEL ZA kiungu SI ZA WATU NDIO MAANA HAWAHESABIWI KAMA WATU.

Hivyo tuache kujidanganya kuwa tutafanikiwa bila mkono wa mwanamke, ukimtunza na ukimtazama kama MSAIDIZI kwa maana ya hapo juu utaiona Eden yako ikistawi sana.

Yalikua mawazo yangu ya redioni tu, leo nimeyakumbuka nimekushirikisha, kwa mliooa wathaminini wake zenu, kwetu ambao bado tunajifunza kuthamini ili muda ukifika tuishi vyema. Mume mtazame mkeo kama Roho Mtakatifu na mke mtazame mumeo kama Kanisa

CantonaJoseph’s contacts

Facebook https://www.facebook.com/CantonaJoseph/

Instagram https://www.instagram.com/Cantona.Joseph.

Twitter https://twitter.com/@CantonaJoseph

LinkedIn https://www.linkedin.com/in/CantonaJo

Management Fortune Baraka Entertainments

Website https://CantonaJoseph.Wordpress.Com

Email:fortunebaraka.entertainmentsltd@gmail.com

cantona.online254@gmail.com

Contacts +254748836127

Wewe ni wa maana sana!

All Rights Reserved @2020/FortuneBarakaEntertainments.


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment