Nigeria: Wanawake kadhaa na watoto watekwa nyara na kundi lenye silaha Kakin

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Nchini Nigeria genge la watu wenye silaha limewateka zaidi ya wanawake 50 wakiwemo watoto katika kijiji cha Kakin Dawa, katika jimbo la Zamfara Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo.

Vikosi vya ulinzi na usalama vinaendelea kupambana na makundi yenye silaha.
Vikosi vya ulinzi na usalama vinaendelea kupambana na makundi yenye silaha. © AP

Polisi na wakaazi wamesema, uvamizi huo utekelezwa Jumapili iliyopita, na watekaji wanadai kikombozi ili kuwaachia huru mateka hao.

Aidha, wakaazi wa kijiji cha Kakin Dawa, wamesema, watu hao wente silaha walikuwa kwenye pikipiki wakati walipotekeleza uvamizi huo.

Wakiwa wamejihami kwa silaha, walipita na kuingia nyumba kwa nyumba, wakitekeleza uhalifu huo kwa mujibu wa polisi na wakaazi hao.

Polisi  katika êneo la Zamfara wamesema vikosi vya ziada tayari vimetumwa   eneo hilo kuweka usalama ,wakati huu raia wakiomba vyombo vya usalama kutuma askari zaidi.

Kwa zaidi ya miaka 15  êneo la kaskazini magharibi mwa Nigeria  limekumbwa na  ukosefu kutokana na uvamizi wa makundi ya kiislamu yanayotaka kujitenga, huku utekaji nyara kwa ajili ya fidia ukiongezeka êneo hilo kutokana pia na umasikini, ukosefu wa ajira na silaha kuwa mikononi mwa watu.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment