Uganda: Kizza Besigye kuendelea kuzuiliwa katika gereza la Luzira hadi Januari 7, 2025

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Kesi ya madai ya kupatikana akiwa na silaha, akiwa jijini Nairobi, nchini Kenya, inayomkabili kiongozi mkongwe wa upinzani nchini Uganda Kizza Besigye na mshirika wake Hajj Obeid Lutale, inayoendelea kwenye Mahakama ya Kijeshi, imeahirishwa hadi tarehe 7 mwezi Januari mwaka 2025.

Mpinzani Kizza Besigye akiwa kwenye sanduku la chuma katika Mahakama Kuu ya Kijeshi ya Uganda huko Makindye, kitongoji cha Kampala, Uganda, Desemba 2, 2024.
Mpinzani Kizza Besigye akiwa kwenye sanduku la chuma katika Mahakama Kuu ya Kijeshi ya Uganda huko Makindye, kitongoji cha Kampala, Uganda, Desemba 2, 2024. REUTERS – Abubaker Lubowa

Hatua hii imekuja baada ya Mawakili wake kusema, upande wa utetezi haujakamilika baada ya Chama cha Mawakili nchini Uganda siku ya Jumatatu, kumyima kibali wakili mashuhuri na mwanasiasa kutoka nchini Kenya, Martha Karua, ni waziri wa zamani wa sheria wa Kenya, ambaye Besigye ameendelea kusisitiza kuwa ni lazima awe Wakili wake mkuu. 

Chama cha Mawakili nchini Uganda kilidai kuwa maombi ya Martha Karua kuongoza timu hiyo yana uchochezi wa kisiasa kuliko ya kitaaluma.

Mwishoni mwa mwezi Novemba, Besigye ambaye amewahi kuwania urais nchini Uganda mara nne, alikamatwa na watu wanaoaminiwa kuwa maafisa wa usalama na kusafirishwa jijini Kampala alikoshtakiwa katika Mahakama ya kijeshi.

Hata hivyo, Martha ameapa kuendelea kuhudhuria kesi ya mahakama ya Besigye akiahidi pia kuiunga mkono timu hiyo ya wanasheria kwa uwezo wowote hata kama sio kama wakili wake.

Kiongozi huyo wa upinzani alitekwa nyara alipokuwa ziarani nchini Kenya mwezi uliopita na kupelekwa kwenye gereza la kijeshi nchini Uganda.

Hatua hiyo ilizua shutuma nyingi na hofu ya mabadilishano ya siri ya taarifa za kijasusi kati ya mataifa hayo mawili jirani.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment