Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Mda mwingine MUNGU huruhusu CHANGAMOTO kubwa kama GOLIATH itokee katika maisha yako…..
…ili umtafute DAUDI mdogo aliyeko ndani mwako.
Uwezo wa MUNGU ulioko ndani mwako ni mkubwa kuliko, VIGEZO ambao wanadamu wataweka juu yako.
Kabla DAUDI hajaanza kupigana na GOLIATH, alipewa kwanza historia yake, kwamba ni JITU kubwa lililoenda hewani, lenye nguvu na lililopigana enzi na enzi.
Huku DAUDI akionekana kuwa ni kijana mdogo wa machungani, asiye na uzoefu yeyote katika mapigano ya kivita.
Watu waliona kuwa DAUDI hana VIGEZO vya kupigana na GOLIATH lakini DAUDI aliona UKUU na UWEZO wa MUNGU ni mkubwa kuliko vigezo vyao.
Lakini, wote tunajua kilichomtokea Goliath.
Katika maisha kuna wakati ambapo unapokuwa unafanya JAMBO fulani,
Watu watakuona kuwa huna UWEZO wa kulifanya kwa sababu ya VIGEZO vyao.
Kitu kikubwa na cha msingi ni kwamba USIKATE tamaa…..
Kwani UWEZO wa MUNGU ni mkubwa kuliko vigezo vyao.
DAUDI hakuwa na uzoefu wa kupigana katika vita kwa kutumia silaha kama mikuki, ngao na mishale,
BALI alikuwa na uzoefu wa kuua SIMBA na DUBI kwa kutumia kombeo.
Kumbuka, wakati anapigana na GOLIATH, alimuua kwa kutumia KOMBEO.

Hivyo usidharau kitu kidogo kile ambacho unaweza kukifanya kwani itakujengea uzoefu ambao ipo siku itakusaidia kufanya jambo kubwa la kushangaza ulimwengu.
ENDELEA KUFANYA.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.