Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Mapigano mapya yameripotiwa katika Mkoa wa Kivu Kaskazini, kati ya wanajeshi wa serikali na waasi.
Mapigano ya hivi karibuni yameripotiwa mwishoni mwa juma, huku hali ya kiusalama ikiendelea kuwa tete katika maeneo muhimu karibu na Goma na sehemu nyingine za mkoa huo.
Kwa mda wa wiki mbili zilizopita, Mkoa wa Kivu Kaskazini umekua n a hali ya utulivu kabla ya Jumamosi na Jumapili, mapigano mapya kutokea tena mjini Sake, mji ulio magharibi mwa Goma.

Vyanzo vya habari vimearifu kua, mabomu yalishuka Jumapili asubuhi karibu na mlima Kimoka, na kufikia sasa idadi ya majeruhi na aina ya silaha zilizotumika bado havijathibitishwa.
Mapigano hayo yanahusisha wanamgambo wa Wazalendo, walioungana na serikali ya Kinshasa, na wapiganaji wa waasi wa M23, ambao inadaiwa wanasaidiwa na Rwanda.
kwa upande mwingine, mapigano yameingia siku ya saba mfululizo katika eneo la Lubero, hasa karibu na Kasegbe, takriban kilomita mia moja kusini mwa Butembo.
Mabadiliko zaidi ya kisiasa na kijeshi yanatarajiwa kama hali itaendelea kuwa tete katika Mkoa wa Kivu Kaskazini.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.