Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Urusi imetangaza kwamba inampa hifadhi aliyekuwa rais wa Syria Bashar Al Assad na familia yake baada ya utawala wake kuanguka, huku Moscow ikisema imefanya hivyo kutokana na sababu za kibinadamu.

Ikulu ya Kremlin inasema kuwa makubaliano yamefikiwa ili kuhakikisha usalama wa kambi za kijeshi za Urusi nchini Syria. Awali Moscow ilisema kambi hizo ziko katika tahadhari kubwa lakini hakukuwa na kitisho dhidi yao kwa sasa.
Assad ameikimbia nchi baada ya waasi kuchukua udhibiti wa mji mkuu Damascus huku akitoa maagizo kwamba ukabidhi wa madaraka ufanyike kwa amani.
Wakati huo huo waasi wa Syria wametangaza marufuku ya watu kutembea nje usiku hadi saa kumi na moja asubuhi. Tangazo hilo limejiri baada ya waasi hao kuchukua udhibiti wa mji mkuu Damascus na kuuangusha utawala wa Bashar Al Assad.
Waasi hao pia wametangaza kwamba rais Assad ameikimbia nchi na kwamba watakabidhi mamlaka kwa Baraza la mpito. Raia wa Syria wameonekana wakimiminika barabarani, wakishangilia baada ya waasi kusitisha utawala wa kiimla wa familia ya Assad wa miaka 50.
Naye Rais wa Marekani Joe Biden amesema ni lazima Assad awajibishwe kwa vitendo vya mauaji na mateso kwa mamia ya maelfu ya Wasyria. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litafanya hivi leo mkutano wa dharura na wa faragha ili kuijadili hali inayoendelea nchini Syria.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.