DRC: Bintou Keita anatoa wito kwa serikali na mashirika ya kiraia kuepuka mivutano zaidi

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Kiongozi wa kikosi cha kudumisha Amani, cha umoja wa mataifa, nchini DRC, Bintou Keita, amewataka wanasiasa na mashirika ya kiraia nchini humo kutochochea hali ya wasi wasi nchini humo.

Kiongozi wa kikosi cha kudumisha Amani, cha umoja wa mataifa, nchini DRC, Bintou Keita,
Kiongozi wa kikosi cha kudumisha Amani, cha umoja wa mataifa, nchini DRC, Bintou Keita, REUTERS – ARLETTE BASHIZI

Akihubia kikao cha baraza la usalama la umoja wa mataifa jijini New York, Bintou Keita, amekiri  hali ya usalama imezidi kuzorota eneo la Kivu Kaskazini tangu mwaka jana, hali hiyo ikichangiwa na mapigano ya makundi ya ya waasi wa  ADFM23, CODECO na Zaire.

Waasi wa M23 wanatuhumiwa kwa kukiuka makubaliano kuhusu usitishwaji wa mapigano mashariki mwa DRC.
Waasi wa M23 wanatuhumiwa kwa kukiuka makubaliano kuhusu usitishwaji wa mapigano mashariki mwa DRC. AP – Moses Sawasawa

Hata hivyo amesema joto la kisiasa linalochangiwa na mjadala kuhusu marekebisho ya katiba, mjadala ulionzishwa na rais Felix Tshisekedi , linachangia hali  ya taharuki.

Amewataka wanasiasa na viongozi wa mashirika ya kiraia kushirikiana na kuendesha mazungumzo kuhusu swala hilo kwa amani ili kutozidisha hali ya wasi wasi.

Bintou Keita amelisisitizia baraza hilo kuunga mkono mikakati ya kurejesha amani nchini DRC, ikiwemo ukamataji silaha .

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment