Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Waendesha mashtaka katika mahakama ya kimataifa ya kushughulikia uhalifu wa kivita, ICC wameitaka mahakama hiyo kuthibitisha kesi dhidi ya viongozi wawili wa kundi la waasi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, lilofahamika kama anti-Balaka.
Waendesha mashtaka katika mahakama ya kimataifa ya kushughulikia uhalifu wa kivita, ICC wameitaka mahakama hiyo kuthibitisha kesi dhidi ya viongozi wawili wa kundi la waasi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, lilofahamika kama anti – Balaka.

Wakitia hoja zao za mwisho katika kesi dhidi ya wawili hao ilionza mwaka 2021, waendesha mashtaka hao, wamesema wana uthibitisho tosha kuwa wawili hao Patrice Edourd Ngaissona na Alfred Yekatom, waliongoza kampeni ya machafuko yaliyolenga raia waislamu.
Mwendesha mashtaka Kweku Vanderpuye, alitupilia mbali utetezi wa upande wa Ngaissona, uliodai kuwa kiongozi huyo wa waasi wa anti Balaka, pia mchezaji wa mpira wa mguu, alijaribu kumaliza machafuko hayo.
Upande wa mashtaka pia ulisema kuwa Yekatom aliyefahamika kwa jina la Rambo alikuwa kiongozi wa waasi hao zaidi ya elfu tatu aliogopwa mno katika kundi hilo, akiwa amewapiga risasi na kuwauwa wapiganaji Wake watatu waliotuhumiwa kuwa wasaliti. Wawili hao hata hivyo walikanusha mashtaka hayo dhidi yao mwaka 2021.
Waasi wa anti-Balaka walianzisha mapigano mwaka 2013 kujibu mauaji na uporaji uliokuwa ukiendesha na waasi wa kislamu wa Seleka waliokuwa wamechukua uongozi mwaka huo.

ICC imekuwa ikichunguza uhalifu wa kivitua nchini Jamhuri ya Kati tangu mwaka 2014 na kuna kesi inayoendelea pia dhidi ya kiongozi wa waasi wa Seleka.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.