Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Mtaalamu wa masuala ya siasa na mwandishi wa insha, raia wa Ufaransa mwenye asili ya Cameroon, Charles Onana, amepatikana na hatia na mahakama ya Ufaransa kwa “kuhusika katika kupinga hadharani kuwepo kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu, katika kesi ya uhalifu wa mauaji ya kimbari” dhidi ya Watutsi, nchini Rwanda.

Charles Onana amekuwa akikabiliwa na mashitaka kutoka kwa mashirika saba yakiwemo Survie, FIDH na LDH, kuhusiana na takriban nukuu ishirini zilizomo katika kitabu chake Rwanda, ukweli kuhusu Operesheni Turquoise – wakati kumbukumbu zinazungumza, kilichochapishwa mnamo 2019.
Mchapishaji wake Damien Serieyx pia amepatikana na hatia ya “kupinga hadharani kuwepo kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu”. Wote wawili watalazimika kulipa faini.
Kwa upande wa mahakama ya Ufaransa, Charles Onana “alipinga”, “alipunguza” na “alifutlia mbali” kwa “njia ya kukasirisha” mauaji ya kimbari ya Watutsi, ambayo yalitokea kati ya mwezi wa Aprili na Julai 1994. Kulingana na uamuzi wa Mahakama, “alidharau” maamuzi yote ya mahakama “yaliyotokana na utambuzi wa kuwepo kwa mauaji haya ya kimbari. “
Hukumu hiyo inaelekeza zaidi kwenye “matumizi mengi sana ya neno “mauaji ya halaiki” – katika alama za nukuu – katika kazi iliyochapishwa na Mfaransa huyo mwenye asili ya Cameroon, “mchakato ambao ndani yake una matamanio yote ya mwandishi kukataa kabisa uwepo wa mauaji ya Watutsi”, kulingana na majakama.
Charles Onana amehukumiwa faini ya siku 120 ya kiasi cha euro 8,400 – ambayo atalazimika kulipa ili kuepuka kufungwa. Mchapishaji wake atalazimika kulipa faini ya euro 5,000.
Wakili wa upande wa utetezi, Emmanuel Pire, amesema “amekatishwa tamaa” na uamuzi huu. Kulingana naye, mteja wake “hapingi mauaji ya kimbari” ya Watutsi katika kitabu chake, lakini “anayaweka katika muktadha” wa wakati huo. Baada uamuzi wa mahakama, alitangaza kwamba atakata rufaa dhidi ya hukumu hii kwa niaba ya mteja wake.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.