Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Wanasiasa wa upinzani nchini Burundi, wamekosoa vikali maagizo ya rais Evariste Ndayishimiye kuhusu uchaguzi wa ubunge ambao umepangwa kufanyika Juni 5 mwaka ujao, wakisema yanalenga kumfungia aliyekuwa kiongozi wa chama cha CNL Agathon Rwasa.

Rais Evariste Ndayishimiye akithibitisha kuandaliwa uchaguzi huo mwaka ujao, ametangaza kanuni za uchaguzi ambazo zinawazuia viongozi wa vyama kuwania kwenye uchaguzi huo au wawe wamejiuzulu au kufurushwa kwenye uongozi kwa muda wa miaka miwili.
Maagizo hayo ya rais yanasisitiza wagombea huru wataruhusiwa kuwania iwapo hawajakuwa wanachama wa chama chochote cha kisiasa kwa muda wa mwaka moja.

Masharti hayo sasa yamepingwa na upinzani wanaosema yameundwa kumzuia moja kwa moja kinara wa chama cha CNL aliyeondolewa, Agathon Rwasa.
Chama cha CNL kiliharamishwa mwezi Agosti na wizara ya usalama wa ndani kufuatia mikutano miwili ya baraza kuu, moja ya mkutano huo ukiwa umesababishwa kuondolewa madarakani Agathon Rwasa.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.