John Dramani Mahama, rais mteule wa Ghana ni nani?

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Mahama mwenye umri wa miaka 66 anaongoza chama cha upinzani cha National Democratic Congress, NDC.
Mahama mwenye umri wa miaka 66 anaongoza chama cha upinzani cha National Democratic Congress, NDC. © Zohra Bensemra / Reuters

John Dramani Mahama ni rais wa zamani aliyehudumu kama rais kati ya mwaka 2012 hadi 2017 na ameshinda uchaguzi huu wa kihistoria na kumfanya kuwa rais wa kwanza nchini Ghana kwa miongo mitatu kurejea madarakani, tangu utawala wa vyama vingi mwaka 1992.

Mahama mwenye umri wa miaka 66 anaongoza chama cha upinzani cha National Democratic Congress, NDC, na wakati wa kampeni aliahidi kuibadilisha Ghana kwa kujadili upya sehemu za mkataba wa shirika la fedha duniani  IMF na kurekebisha uchumi wa “saa 24” ili kuunda nafasi za kazi.

Ni mwandishi wa kitabu chake cha “My First Coup d’Etat akihadidthia mambo aliyopitia wakati wa mapinduzi ya kijeshi mwaka 1966. Na wakati wa kampeni alitetea uongozi wake kutokana na uzoefu wake katika uongozi wa kimataifa.

Kuhusu swala la ufisadi ambalo liligubika utawala wake alipokuwa rais licha ya kutofunguliwa mashtaka rasmi, Mahama, amesema atabuni ofisi mpya itakayowajibisha serikali kuhusu zabuni zinazotolewa

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment