Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
1. ACHA KUJITAMKIA MANENO MABAYA.
Maneno ni mbegu, Kila unachojitamkia unakipa uhai, na ipo siku utavuna matunda yake.
Jitamkie maneno yenye nguvu, yenye hamasa na yenye kukuletea mtazamo chanya.
3. ACHA KUJIWAZIA MABAYA.
Kila kitu huanzia katika fikra za mtu. Ukijiwazia mambo mabaya, yatatokea. Ukiwaza mazuri yatatokea.
Ni kweli Kuna vitu vipo nje ya uwezo wetu lakini, akili zetu ni kama sumaku, huvuta matokeo ya kile tunachokiwaza upande.
Think positive, you beautiful, you are talented and genius.
3. ACHA KUJIDHARAU.
Usijione haufai, hauwezi kitu wala wewe huna issue yeyote. Kumbuka hali uliyonayo Sasa, siyo ukomo wa maisha yako.
Within a. Second, GOD can change your life.
Sisi binadamu Kuna muda tunajihisi hatufai lakini, Mungu ana sababu kuu kwanini uko hai mpaka Leo.
4. ACHA KUISHI KWENYE MATATIZO YAKO.
Hakuna siku Dunia itasimama kulia au kukuonea huruma.
Kwa sababu kila MTU ana matatizo yake ila tunatofautiana jinsi kila mtu anavyochukulia matatizo yake.
Don’t take it personal!
Kila mtu anapambana na hali yake katika changamoto na matatizo yake. Usiishi kwenye matatizo, take them as a challenge to next level.
5. ACHA KUJIDANGANYA.
Be honest to yourself!
Mara nyingi sana tunadanganya nafsi zetu ili kuwafurahisha wengine.
Inafika mahali tunajifanya tunafuraha kumbe ndani tunalia.
Yes! Hatupaswi, kunyong’onyea lakini iwe katika uhalisia.
Usijadanganye kwa lolote Kwa ajili ya watu wengine.
NO! Kwa sababu siku ukipewa kisogo, utajutia zaidi.
6. ACHA KUJIAMBIA HAUKO TAYARI.
Kila mara fursa zinaginga mlangoni kwako, unasema Kwa Sasa sipo tayari.
Zinagonga tena na Tena, bado unasikia sauti kutoka ndani, …”ACHA BANA HAUKO TAYARI”.
Hakuna mtu ambaye amewahi kuwa tayari kwa 100% wakati wa kuanza kitu chochote.
Hivyo, ukitanguliza EXCUSES Sana za kutokuwa tayari, basi FURSA nyingi zitapita kushoto kwako.
7. ACHA KUTEGEMEA WATU KWA 100%
Mtu atakuambia nitakutafutia kazi alafu baada ya muda kimya.
Nitakupa hiki alafu akiona simu yako hapokei.
YES!! Na wao ni binadamu na wao wanapigana vita vyao tusiyoyajua.
Hivyo, usiwatushe mzigo wako Kwa asilimia 100%. Utakuwa disappointed Sana!
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.