Mali: Wapinzani 11 dhidi ya utawala wa kijeshi waachiliwa kwa muda

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Miezi mitano baada ya kukamatwa nyumbani kwa mmoja wao kwa kufanya mkutano wa kisiasa kinyume cha sheria, wapinzani 11 wa utawala wa kijeshi nchini Mali wameachiliwa kwa muda siku ya Alhamisi hioni, Desemba 5. Mawaziri kadhaa wa zamani na viongozi wa chama waliotia saini tamko la kuitaka serikali kurudisha madaraka kwa raia ni miongoni mwao. Uamuzi wa mahakama ambao pia unazingatia hali ya kisiasa.

RFI Afrique / Carte pays : Mali et sa capitale Bamako.
非洲国家 / 马里及其首都巴马科(Bamako)。 Mawaziri kadhaa wa zamani na viongozi wa vyama vya siasa waliotia saini jukwaa la kutaka kurejea kwa utaratibu wa kikatiba ni miongoni mwa wapinzani 11 walioachiliwa huru nchini Mali. © FMM Studio graphique

Ndugu na marafiki zao wa karibu ambao tayari wameweza kukutana nao wana kauli moja: wapinzani 11 wa kisiasa wa utawala wa kijeshi  nchini Mali walioachiliwa kwa muda siku ya Alhamisi hii, Desemba 5 wamechoka sana lakini hawajapata mateso ya kimwili ya kudhalilisha wakiwa kizuizini. Basi dogo ambalo wafungwa wa zamani wamesafiria wakati wakitoka gerezani katika mji wa Kéniéroba limefika Bamako baada ya takriban saa mbili.

Wakiwasilishwa mara moja kwa jaji wa mahakama ya Commune V ya mji mkuu wa Mali, waliweza kusoma maelezo ya agizo lao la kuachiliwa huru: bila kuwekwa chini ya masharti ya mahakama, wako huru kusafiri popote wanapotaka .

Walipotoka mahakamani, walikutana kwa muda mfupi na Waziri Mkuu wa zamani ambaye alifanya usuluhishi. Kulingana na waziri wamkuu huyu wa zamani, kuachiliwa kwao “pia ni ishara ya utulivu wa kisiasa na iko ndani ya mfumo wa upatanisho wa kitaifa” unaotarajiwa na utawala wa kijeshi.

Wanachama wa jukwaa ambalo linadai kutoka kwa jeshi kurejea kwa utaratibu wa kikatiba, wapinzani 11 walioachiliwa Alhamisi hii walikamatwa mwezi Juni wakati walishiriki katika mkutano wa kisiasa ulioandaliwa katika nyumba ya kibinafsi ya mmoja wao. Kisha walikamatwa kwa “mkutano usioidhinishwa” wakati ambapo shughuli za chama zilipigwa marufuku – hatua ambayo iliondolewa tangu wakati huo. Wote walikaa gerezani kwa zaidi ya miezi mitano.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment