Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Nchini Korea Kusini, tangu kutangazwa kwa sheria ya kijeshi na kuifuta, maandamano yameendelea katika mitaa ya Seoul. Hata leo, raia wa Korea Kusini wamekusanyika katikati mwa jiji kutaka rais ajiuzulu, akilengwa na uchunguzi wa polisi kwa uhaini baada ya mapinduzi yake ya kijeshi. Hoja ya kumuondoa madarakani pia itapigiwa kura kesho bungeni. Wakati huo huo, maafisa watatu wakuu wa jeshi la Korea Kusini wamesimamishwa kazi.
Kila siku, maelfu ya Wakorea Kusini hukusanyika katikati mwa jiji au mbele ya Bunge la Ktaifa kumtaka Rais Yoon Suk-yeol ajiuzulu, anaandika mwandishi wetu wa Seoul, Celio Fioretti. Akiwa ametengwa zaidi, anaweza kuwa anaishi saa zake za mwisho kama mkuu wa nchi. Chama chake kimetangaza leo asubuhi kwamba kitapiga kura kuunga mkono hoja ya kumuondoa madarakani siku ya Jumamosi, Desemba 7. Uamuzi ambao unakuja baada ya ufichuzi ambao Rais Yoon aliamuru kukamatwa kwa wapinzani siku ya Jumanne jioni, ikiwa ni pamoja na ndani ya kambi yake mwenyewe.
Kuondolewa kwenye wadhifa wake
Ikiwa hoja hii itaidhinishwa, Bw. Yoon atasimamishwa kazi akisubiri uthibitisho wa kutimuliwa kwake na Mahakama ya Kikatiba. Iwapo majaji watidhinisha hilo, uchaguzi mpya wa urais utafanyika ndani ya siku sitini, linaripoti shirika la habari la AFP. Kipindi cha mpito kitasimamiwa na Waziri Mkuu Han Duck-soo. Bw. Yoon, ambaye hajaonekana hadharani tangu siku ya Jumatano asubuhi, pia ndiye mlengwa wa uchunguzi wa polisi kwa “uasi”.
Mwandamanaji huyu anasubiri uamuzi wa kura ya kesho: “Kwa siku ya Jumamosi, nadhani kila mtu hapa anasubiri jambo moja tu na mimi pia, kwamba utawala wa Yoon Suk-yeol utaanguka na kujiuzulu . Hili ndilo suluhisho pekee la mgogoro huu. “
Profesa huyu – aliyegoma – pia alikuja kushiriki katika mkutano huo: “Rais amezindua mapinduzi, haikubaliki. Tunatoa wito kwa Yoon Suk-yeol kujiuzulu, ndiyo maana tuko hapa leo. Mimi ni mwalimu na baadhi yetu tunagoma leo kumpinga rais. Hata hivyo, tangu Desemba 3, wananchi wamekuwa wakikusanyika kila siku, na kesho ikiwa ni mwishoni mwa wiki, nadhani wananchi wengi zaidi watakuja. Tutamshusha kwa nguvu za watu. Licha ya kushikilia madaraka na kutaka kusalia madarakani kwa nguvu, itabidi wananchi waingilie kati wenyewe. Hivi ndivyo historia ya nchi yetu ilivyoandikwa. “
Jeshi litakataa maagizo mapya ya Yoon Suk-yeol
Uvumi unaenea kuhusu uwezekano wa kurejeshwa kwa sheria ya kijeshi ili kuzuia kura ya kumuondoa madarakani. Lakini wakuu wa majeshi wamebainishwa kwamba wamekataa maagizo yoyote mapya kutoka kwa rais kulinda nchi. Maafisa watatu wakuu wa jeshi la Korea Kusini wamesimamishwa kazi kwa kushiriki katika operesheni wakati wa sheria ya kijeshi ya muda mfupi, Wizara ya Ulinzi pia imetangaza siku ya Ijumaa. Huyu ni kamanda wa kijeshi wa Seoul, yule wa kikosi maalum na kile cha kukabiliana na ujasusi, imebainisha wizara hiyo katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyochukuliwa na shirika la habari la AFP.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.