Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Kwa mara nyingine umoja wa Mataifa umeonya kuhusu hali mbaya ya kibinadamu inayoshuhudiwa na itakayoendelea kushuhudiwa nchini Sudan, wakati huu tayari hali ya njaa ikiwa imetangazwa kwenye taifa hilo.

Mwezi Juni, kamati maalumu ya umoja wa Mataifa inayofuatilia mwenendo wa upatikanaji wa chakula duniani, ilisema watu zaidi ya laki 7 nchini humo wanakabiliwa na baa la njaa na kwamba kunahitajika udharura wa kushughulikia mzozo unaoendelea.
Tayari mashirika kadhaa ya kibinadamu ya umoja wa Mataifa na yale washirika, wametangaza njaa kwenye kambi kubwa zaidi ya wakimbizi ya Zamzam, ambako wapiganaji wa RSF wanaendeleza mashambulio.

Juma lililopita, umoja wa mataifa kupitia ofisi yake ya kuratibu misaada ya kibinadamu, OCHA, ulisema licha ya kufanikiwa kufikisha misaada katika baadhi ya maeneo ambako raia wanahitaji msaada wa dharura, kulihitajika juhudi za ziada kuwafikia watu mamilioni ya raia ambao wanaendelea kukimbia machafuko.

Haya yanajiri wakati huu ambapo jeshi la Serikali na wapiganaji wa RSF, wote hawaoneshi nia wala utayari wa kuzungumza kwa uwazi ili kumaliza vita na kupata suluhu ya mzozo wa kisiasa unaoendelea licha ya shinikizo toka jumuiya ya kimataifa.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.