DRC: Mahakama Kuu ya Kijeshi yathibitisha hukumu ya kifo dhidi ya Corneille Nangaa na wengine 5

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Mahakama ya kijeshi kwenye mji wa Ndolo nchini DRC, imethibitisha adhabu ya kifo waliyopewa washirika watano wa aliyewahi kuwa mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini humo, Corneille Nangaa, ambaye kwa sasa anaongoza vuguvugu la Alliance Fleuve Congo.

Washtakiwa katika mahakama ya kijeshi huko Goma, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Septemba 15, 2023.
Washtakiwa katika mahakama ya kijeshi huko Goma, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Septemba 15, 2023. © Alexis Huguet / AFP

Katika kesi hio, wahusika watano waliopewa hukumu hiyo ni Eric Nkuba Shebandu, Samafu Makinu Nicaise, Nangaa Baseyane Ruttens, M’Kangya Nyamatshaba na Safari Bishori Luc.

Kulingana na hukumu, watano hao, walipatikana na makosa ya uhalifu wa kivita, mauaji ya kukusudia, uharibifu wa mali na ushiriki katika harakati za uasi uliofanywa na wasaidizi walio chini ya mamlaka yao.

Washtakiwa katika mahakama ya kijeshi huko Goma, mashariki mwa DRC.
Washtakiwa katika mahakama ya kijeshi huko Goma, mashariki mwa DRC. Reuters/Kenny Katombe

Hata hivyo wataalamu wa sheria wanasisitiza kuwa, ingawa hukumu ya kifo imethibitishwa, bado kuna njia ya kupinga kupitia rufaa mbele ya Mahakama ya juu.

Aidha Corneille Nangaa na wenzake 20 ambao walihukumiwa bila kuwepo mahakamani, wataendelea kusubiri baada ya Mahakama Kuu ya Kijeshi Kusitisha mchakato wa rufaa dhidi yao.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment