UNICEF yazindua mpango wa kuwasaidia watoto walioathirika na mizozo duniani

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Shirika la watoto duniani, UNICEF, limezindua mpango wa kuchangisha kiasi cha dola za Marekani bilioni 9.9 kwa ajili ya mwaka ujao ili kutoa msaada kwa mamilioni ya vijana na watoto walioathiriwa na vita pamoja na mizozo mingine duniani.

Watoto wengi haswa katika mataifa yenye mizozo wameathirika zaidi ikiwemo maeneo kama vile Gaza.
Watoto wengi haswa katika mataifa yenye mizozo wameathirika zaidi ikiwemo maeneo kama vile Gaza. REUTERS – IBRAHEEM ABU MUSTAFA

Kwa mujibu wa UNICEF, fedha hizi zitasaidia katika majibu ya dharura kwa migogoro mbalimbali ikiwemo mabadiliko ya tabianchi, uhamiaji, na matatizo ya kiafya yanayotarajiwa mwaka ujao.

Kwa sasa, watoto milioni 213 duniani wanakabiliwa na hali ngumu kutokana na vita na mabadiliko ya hali ya hewa, huku UNICEF ikikusudia kuwafikia watoto milioni 109, hii ikiwa ni idadi kubwa ya watoto ambao wanahitaji huduma za msingi kama vile afya, elimu, na maji safi.

Watoto milioni 213 duniani wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha.
Watoto milioni 213 duniani wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha. AP – Rajanish Kakade

Mwaka huu, zaidi ya watoto milioni 57.5 walizaliwa katika maeneo yaliyoathiriwa na migogoro, na idadi hii inatarajiwa kuongezeka kwa watoto 400,000 zaidi mwaka ujao.

Barani Afrika, Miongoni mwa nchi zitakazohitaji msaada wa shirika hili ni pamoja na sudan kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment