FURAHA YAKO IKO WAPI (WHERE IS YOUR HAPPINESS)

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Kila mtu anapenda kufurahi, na kila mtu anapenda kuishi maisha yenye FURAHA. Masaa, siku, miezi na miaka haifanani, hivyo mwanadamu katika maisha yake hupitia nyakati tofauti tofauti ambazo pengine huweza kumfanya afurahi zaidi au furaha yake kuwa chini.

Katika hali ya namna hii tunawapata watu wa makundi mawili.

1. Kundi la kwanza ni watu ambao, FURAHA yao ni matokeo ya vitu walivyonavyo . Yaani, chanzo cha furaha ni kwa sababu ya vitu alivyonanvyo. Ni kweli kila mtu hufurahi pale anapofanikisha au anapokipata kitu anachokipenda zaidi, au alichotumia nguvu na juhudi nyingi kukipata, NA kimsingi ni vyema kufanya hivyo kwa sababu ni sehemu ya kujipongeza mwenyewe na kujikubali. Lakini kwa upande mwingine wa shilingi, inatupasa kuwa makini kwa sababu FURAHA ya aina hii ni pale tu, utakapopata matokeo uliyotegemea. Katika maisha kuna kipindi mambo hutokea kinyume na matarajio yetu, hivyo mtu huweza kujikuta hana furaha na matokeo hayo, na kujikuta akijutia, akihuzunika na kujilaumu. Kitu cha msingi ni kujitahidi kuwa na furaha, hata pale tunapofeli, kwani itakufanya kuamsha NGUVU kubwa iliyopo ndani mwako, na HAMASA ambayo itakuwa chachu ya kusimama tena na kusonga mbele. Watu wa aina hii ndio Wale ambao, wakati wanafanya vitu kwa juhudi zao, hawapati furaha mpka wapate matokeo wanayoyataka.

2. Kundi la pili ni watu ambao, FURAHA yao ndio chachu ya matokeo wanayopata. Yaani hawasubiri wawe na vitu ili wafurahi, bali FURAHA yao ni KIINI cha mambo wanayoyafanya au matokeo wanayoyapata. Kimsingi ukifanya jambo ukiwa unalifurahia, hautakuwa na HOFU juu yake, bali FURAHA yako itakupa mwamko, nguvu na hamasa kubwa ya kufanya katika namna endelevu, na kukufanya ukubaliane na hali yeyote utakayokumbana nayo mbeleni. Watu wa aina hii ndio, Wale tunaowaona kila siku wakiwa na FURAHA, hata kama wanaungulia katika chungu cha changamoto na matatizo.

Kitu cha msingi ni kwamba, FURAHA inatoka ndani ya mtu mwenyewe, ndio maana hata mtoto mdogo ambaye hana kitu chochote mda wote hupenda kufurahi. Furaha haitokani katika vitu, wapo watu wenye kila kitu unachokijua duniani lakini FURAHA kwao ni kama hadithi, huishia kuona na kusikia kwa wengine.

Jifunze kufurahi kwa kile ulichojaliwa nacho, uwezo ulionao na katika jambo unalolifanya.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment