Mataifa yashindwa kufikia makubaliano katika mazungumzo ya plastiki ya Umoja wa Mataifa

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Mkutano wa umoja wa Mataifa kuhusu taka za plastiki uliokuwa unafanyika kwenye mji wa Busan nchini Korea Kusini, umetamatika jana jioni huku wajumbe wakishindwa kufikia makubaliano ya mkataba wa kidunia kuhusu udhibiti wa taka za plastic, ambapo wamekubaliana kuongeza muda wa majadiliano.

Wanaharakati wa mazingira wanaonyesha ishara ya kukabiliana na taka za plastiki katika ufuo mjini Busan, South Kusini, Nov. 24, 2024. (Son Hyung-joo/Yonhap via AP)
Wanaharakati wa mazingira wanaonyesha ishara ya kukabiliana na taka za plastiki katika ufuo mjini Busan, South Kusini, Nov. 24, 2024. (Son Hyung-joo/Yonhap via AP) AP – Son Hyung-joo

Kwa karibu wiki moja, wanadiplomasia toka mataifa karibu 200 walikuwa wakijaribu kutafuta muafaka wa pamoja kuhusu namna ya kukabiliana na athari za taka za plastiki.

Katika kongamano hili, mataifa ya Afrika yalikuwa yanaunga mkono kupatikana kwa mkataba wa kidunia kudhibiti taka za plastiki, lakini zikakutana na upinzani toka mataifa ambayo ni wazalishaji wakubwa wa mafuta ya Visikuku, yanayopinga azimio lolote la kusitisha uzalishaji wa plastic.

Miongoni mwa masuala tata yaliyokwamisha makubaliano ni pamoja na nivipi kutakuwa na udhibiti wa uzalishaji wa plastiki zisizo na tija, aina ya kemikali zinazotumiwa, ufadhili wa kifedha kwa nchi masikini pamoja na kuwa na sheria ya kimataifa itakayofuatwa na mataifa yote duniani kuhudu taka za plastiki.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment