Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Hofu yatanda kufuatia vifo vya watu wengi huko N’Zérékoré, kusini-mashariki mwa Guinea, baada ya msongamano wa watu kwenye uwanja wa michezo wa jiji hilo. Hakuna takwimu za kuaminika hadi sasa, lakini picha na video zinazozunguka zinaonyesha maiti nyingi na majeruhi wengi. Fainali ya mashindano ya kandanda ya “Jenerali Mamadi Doumbouya” ilizua taharuki katika dakika za mwisho. Vijana na polisi walihusika, na kusababisha hali ya machafuko.

Ilikuwa katika dakika za mwisho za za mchezo wa fainali ya kombe la “Jenerali Mamadi Doumbouya” kati ya timu ya N’Zérékoré na ile ya Labé, katika uwanja uliokuwa umejaa watu na mbele ya wajumbe wa serikali, wakati muamuzi alipoadhibu kosa kwa mkwaju wa penalti kwa faida ya timu N’Zérékoré.
Wachezaji wa timu ya Labé na mashabiki wao walipinga kosa hilo, wakamshambulia mwamuzi, mzozo ulianza wakati uwanja ukiwa umevamiwa: kulingana na mashahidi, polisi kisha walirusha mabomu ya machozi. Vijana wakajibu kwa kurusha mawe. Makabiliano hayo yalisababisha msongamano wa watu kuelekea kwenye njia moja pekee ya kutoka kwenye uwanja huo.
Vyanzo kadhaa kwenye eneo la tukio vinasema wanahofia kuwa idadi ya vifo ni kubwa. Picha na video zinazosambaa zinaonyesha maiti nyingi zikiwa uwanjani na kwenye korido za hospitali ya mkoa, ambapo daktari mmoja amezungumza juu ya vifo kadhaa na makumi ya majeruhi kutibiwa.
Hadi wakati huo, mashindano hayo yalikuwa ya sherehe, yakivutia maelfu ya watu. Matukio kadhaa ya aina hii kwa jina la mkuu wa utawala wa kijeshi yameandaliwa tangu katikati ya mwezi Septemba katika mikoa, ili kuandaa kugombea kwake kwa uchaguzi ujao wa urais, wapinzani wake wanabainisha.
Bah Oury, Waziri Mkuu wa mpito ameandika ujumbe kwenye mtandao wa X ambapo amesema “serikali inachukizwa na matukio ambayo yameharibu mechi”. Anathibitisha kwamba kuna “waathirika”. Bah Oury anaongeza kuwa “mamlaka za kikanda zinafanya kazi kwa bidii ili kurejesha utulivu miongoni mwa wakazi. Mamlaka za maadili za jiji zinaombwa pia kuchangia katika kurejesha utulivu wa kijamii”.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.