AFRIKA LEO JIONI.–29-11-2024

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Karibu katika Matangazo yetu ya jioni moja kwa moja kutoka Communication Center. Tumekuandalia mengi ikiwa ni pamoja

Muhtasari

Naam,Natumai U buheri wa afya popote pale ulipo duniani kwa mwoyo mkunjufu na mikono miwili Hujambo na karibu katika matangazo yetu Afrika Leo Jioni ya moja kwa moja ikiwa ni tarehe 29/11/2024 Jina langu ni Cantona Joseph,karibu.

Chama cha ACT wazalendo chataka uchaguzi wa serikali za mitaa urudiwe

Chama cha upinzani cha ACT Wzalendo nchini Tanzania kimetaka uchaguzi wa serikali za Mitaa urudiwe na matokeo yaliyotangazwa na Wizara ya TAMISEMI kufutiliwa mbali.

“ACT hatukubaliani na matokeo yaliyotangazwa na Waziri wa TAMISEMI, kwani mchakato mzima wa uchaguzi umevurungwa kwa kiwango ambacho kimepora madaraka ya wananchi kuchagua viongozi wao,’ imesema sehemu ya taarifa ya chama hicho.

Serikali kupitia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ilitangaza matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika hivi karibuni, ambapo chama kinachoongoza nchi, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimeshinda kwa asilimia 98.8, kikiibuka na ushindi wa nafasi 4,213 katika nafasi za serikali za mitaa.

Kwa upande mwingine, chama kikuu cha upinzani, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeshinda nafasi 36 pekee, sawa na asilimia 0.84 ya jumla ya nafasi zilizogombewa.

Matokeo hayo yanakuja baada ya malalamiko kutoka kwa baadhi ya vyama vya upinzani, wakiwemo viongozi wa Chadema, ambao wamekosoa mchakato wa uchaguzi.

Chadema inadai kwamba uchaguzi huo haukuzingatia misingi ya demokrasia, huku wakitaja kuwa baadhi ya wananchi walikosa haki ya kupiga kura kwa sababu ya kutokuwepo kwa majina yao kwenye daftari la wapigakura. Aidha, Chadema wameeleza kuwa baadhi ya wagombea wao walikumbwa na vitendo vya vurugu, wakiwemo viongozi wao waliouawa.

Matokeo ya Uchaguzi wa serikali za Mitaa Tanzania yatangazwa,

g
Maelezo ya picha,Waziri wa Tamisemi Mohammed Mchengerwa

Serikali kupitia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imetangaza matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika hivi karibuni, ambapo chama kinachoongoza nchi, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimeshinda kwa asilimia 98.8, kikiibuka na ushindi wa nafasi 4,213 katika nafasi za serikali za mitaa.

Kwa upande mwingine, chama kikuu cha upinzani, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeshinda nafasi 36 pekee, sawa na asilimia 0.84 ya jumla ya nafasi zilizogombewa.

Matokeo hayo yanakuja baada ya malalamiko kutoka kwa baadhi ya vyama vya upinzani, wakiwemo viongozi wa Chadema, ambao wamekosoa mchakato wa uchaguzi.

Chadema inadai kwamba uchaguzi huo haukuzingatia misingi ya demokrasia, huku wakitaja kuwa baadhi ya wananchi walikosa haki ya kupiga kura kwa sababu ya kutokuwepo kwa majina yao kwenye daftari la wapigakura. Aidha, Chadema wameeleza kuwa baadhi ya wagombea wao walikumbwa na vitendo vya vurugu, wakiwemo viongozi wao waliouawa.

Hadi sasa, Serikali haijatoa majibu yoyote kuhusu tuhuma hizo.

g
Maelezo ya picha,Mwanamke akipiga kura katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, akizungumza na BBC, amesema chama chake kinakusanya taarifa kuhusu mwenendo wa uchaguzi na kwamba watatoa taarifa rasmi kwa umma kuhusu hatua watakazochukua.

Kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi, chama au mgombea ambaye hakuridhika na matokeo ya uchaguzi ana haki ya kuwasilisha malalamiko yake katika Mahakama za Wilaya kwa ajili ya kupinga matokeo hayo.

Uchaguzi wa serikali za mitaa nchini Tanzania kihistoria umekumbwa na changamoto, ikiwa ni pamoja na madai ya kasoro. Uchaguzi huu na ule wa 2019, kwa mfano, uligubikwa na kuenguliwa kwa wingi kwa wagombea wa upinzani, jambo lililosababisha vyama vikuu kama vile CHADEMA mwaka 2019 kususia. Historia hii imeweka kivuli kwenye chaguzi zingine, huku vyama vya upinzani vikitaka uangalizi mkubwa zaidi ili kuhakikisha haki inatendeka.

Vilevile vyama vya upinzani vimeibua wasiwasi kuhusu ushiriki wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) katika kusimamia uchaguzi.

Wanasema kuwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) inapaswa kusimamia chaguzi hizi, kwa kuzingatia sheria mpya za uchaguzi zilizopitishwa. Vyama hivi vinataja matukio ya awali, kama vile madai ya udukuzi wa kura na kuenguliwa kwa wagombea, kuwa ni sababu za kutoaminiana.

Hatahivyo akjibu tuhuma hizo, Waziri Mohamed Mchengerwa, (TAMISEMI}, amesema suala la kuenguliwa sio la upendeleo bali ni utekelezaji wa kanuni kwani hata wagombea wa CCM walienguliwa.

Waziri huyo amevionyooshea kidole cha lawama baadhi ya vyama vya upinzani akisema vinafanya propaganda kwa kusambaza taarifa kwenye mitandao ya kijamii huku wagombea wao wakiwa nyumbani badala ya kufuata utaratibu wa kukata rufaa kama kanuni zinavyotaka.

Israel yaonya raia dhidi ya kurejea katika vijiji 60 vya Lebanon

th

Jeshi la Israel limewaonya raia wa Lebanon kutorejea katika vijiji 60 kusini mwa nchi hiyo, siku tatu baada ya kusitishwa kwa mapigano baada ya zaidi ya mwaka mmoja wa mapigano na kundi la wapiganaji la Shia la Hezbollah.

Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) lilichapisha ramani inayoonyesha eneo lenye kina cha maili kadhaa, ambalo lilisema wakazi hawapaswi kurudi. Yeyote atakayefanya hivyo, lilisema, atakuwa anajiweka hatarini.

Zaidi ya Walebanon milioni moja wamekimbia makazi yao kutokana na mapigano hayo, wengi wao kutoka kusini. Makumi ya maelfu ya Waisraeli pia wameyakimbia makazi yao.

Usitishaji wa mapigano ulianza kutekelezwa Jumatano asubuhi, ingawa maafisa wa Israeli na Lebanon wameshtumu kila mmoja kuwa tayari amekiuka.

Siku ya Alhamisi, IDF ilisema vikosi vyake vilifyatua mizinga na kufanya mashambulizi ya anga dhidi ya wappiganaji kusini mwa Lebanon.

Iliongeza kuwa iliwafyatulia risasi washukiwa baada ya kuona shughuli katika kituo cha silaha cha Hezbollah, na magari yakiwasili katika maeneo kadhaa, ambayo ilisema yalikiuka usitishaji mapigano.

Lebanon iliishutumu Israel kwa kukiuka makubaliano “mara kadhaa” na kusema inafuatilia hali hiyo.

Chad yasitisha makubaliano ya kijeshi na Ufaransa

Takriban wanajeshi 1,000 wa Ufaransa kwa sasa wako nchini Chad
Maelezo ya picha,Takriban wanajeshi 1,000 wa Ufaransa kwa sasa wako nchini Chad

Chad imesema inasitisha makubaliano muhimu ya ushirikiano wa kiulinzi na Ufaransa, na hivyo kuzua maswali kuhusu kupungua kwa ushawishi wa Paris katika eneo linalokabiliwa na mzozo la Sahel barani Afrika.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Chad Abderaman Koulamallah alisema ni wakati wa nchi yake “kudai mamlaka yake kamili”.

Tangazo hilo limekuja saa chache baada ya mwenzake wa Koulamallah wa Ufaransa, Jean-Noel Barrot, kukutana na Rais wa Chad Mahamat Deby.

Chad ni mshirika mkuu katika mapambano ya nchi za Magharibi dhidi ya wanamgambo wa Kikijihadi katika eneo la Sahel huko Afrika Magharibi.

Lakini kabla ya uchaguzi wa rais mwezi Mei, mamlaka ya Chad iliamuru kuondolewa kwa wanajeshi wa Marekani nchini humo, kuashiria kujiwtengai na washirika wa jadi wa nchi hiyo wa Magharibi.

Ufaransa kwa sasa ina takriban wanajeshi 1,000 katika nchi hiyo ya Afrika ya Kati wanayotoa usaidizi wa kijasusi na vifaa kwa wanajeshi wa Chad kutoka katika kambi zao, ukiwemo katika mji mkuu N’Djamena.

Ufaransa, mtawala wa zamani wa kikoloni wa Chad, alikuwa ametia saini toleo lililorekebishwa la makubaliano ya kijeshi na usalama mnamo 2019.

Mashirika ya ndege ya India yamekumbwa na vitisho 1,000 vya uongo vya mabomu

xx

Mashirika ya ndege na viwanja vya ndege vya India vilipokea vitisho 999 vya uongo mashambulio ya mabomu mwaka huu kufikia tarehe 14 Novemba, naibu waziri wa usafiri wa anga wa nchi hiyo aliliambia bunge lake.

Hii ilikuwa karibu mara 10 zaidi ya vitisho vilivyopokelewa mnamo 2023, Bw Murlidhar Mohol alisema.

Zaidi ya vitisho 500 vya mwaka huu vilipokelewa katika wiki mbili zilizopita za mwezi Oktoba.

Ongezeko kubwa la vitisho vya uongo lilikuwa limesababisha uharibifu kwenye ratiba za ndege, na kusababisha usumbufu mkubwa katika mpango wa utoaji huduma.

Vitisho vya hivi majuzi vyote ni uwongo, Bw Mohol alisema, na “hakuna tishio halisi lililogunduliwa katika viwanja vya ndege nchini India”.

Polisi wamepokea malalamiko 256 na watu 12 wamekamatwa kuhusiana na vitisho hivi, waziri alisema.

Lakini visa hivyo vinaashiria ongezeko ambalo halijawahi kushuhudiwa vya matukio kama hayao.

Kati ya 2014 na 2017, viongozi walikuwa wamerekodi arifa 120 za uongo za mabomu kwenye viwanja vya ndege, na karibu nusu zilielekezwa Delhi na Mumbai, viwanja vya ndege vikubwa zaidi nchini.

China yamfunga mwandishi wa habari aliyepatikana na hatia ya ujasusi

xx

Mwanahabari wa zamani wa vyombo vya habari vya serikali ya China amehukumiwa kifungo cha miaka saba jela kwa kosa la ujasusi, familia yake imethibitishia kwa BBC.

Dong Yuyu, 62, ambaye amekuwa kizuizini tangu 2022, alikuwa akifanya kazi katika nchini Marekani na Japan na alikutana mara kwa mara na wanadiplomasia wa kigeni.

Alikuwa akila chakula cha mchana na mwanadiplomasia wa Japan mjini Beijing alipokamatwa na polisi.

Wakati wa kuzuiliwa kwake, Dong alikuwa mfanyakazi mkuu wa gazeti la Guangming Daily, mojawapo ya magazeti makuu matano yanayohusishwa na Chama cha Kikomunisti cha China.

Mnamo Februari 2022, Dong alikamatwa akiwa anakula chakula cha mchana na mwanadiplomasia wa Japan siku moja baada ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi kumalizika huko Beijing, kwenye mgahawa ambapo mara nyingi alikuwa akikutana na marafiki wa kigeni.

Mwanadiplomasia huyo pia alizuiliwa – kisha akaachiliwa saa kadhaa baadaye huku kukiwa na maandamano kutoka kwa serikali ya Japan.

Ajali mbaya yazua lawama kuhusu programu elekezi ya Google map

g
Maelezo ya picha,Wanaume hao watatu walikuwa wakielekea harusini ajali ilipotokea

Je, programu ya urambazaji inaweza kuwajibika ikiwa mtumiaji anapata ajali?

Hilo ndilo swali linaloulizwa nchini India baada ya wanaume watatu kufa wakati gari lao lilipotoka kwenye daraja ambalo halijakamilika na kuangukia kwenye kingo za mto katika jimbo la kaskazini la Uttar Pradesh.

Polisi bado wanachunguza tukio hilo lililotokea siku ya Jumapili, lakini wanaamini kuwa Ramani za Google ziliongoza kundi hilo kutumia barabara hiyo.

Sehemu ya daraja hilo iliripotiwa kuporomoka mwanzoni mwa mwaka huu kwa sababu ya mafuriko na wakati wenyeji walijua hilo na kulikwepa daraja hilo, watu hao watatu hawakufahamu hilo na walikuwa wanatoka nje ya eneo hilo. Hakukuwa na vizuizi au mabango ya ishara zinazoonyesha kwamba daraja lilikuwa halijakamilika.

Mamlaka imewataja wahandisi wanne kutoka idara ya barabara ya jimbo hilo na afisa ambaye jina lake halikutajwa kutoka Ramani za Google katika malalamiko ya polisi kwa tuhuma za kuua bila kukusudia.

Msemaji kutoka Google aliambia BBC Idhaa ya Kihindi kuwa inashirikiana na uchunguzi huo.

Ajali hiyo mbaya imeangazia miundombinu duni ya barabara nchini India na kuzua mjadala kuhusu iwapo programu za urambazaji kama vile Ramani za Google zinashirikishwa katika uwajibikaji kwa matukio kama haya.

Wengine wanailaumu programu hiyo kwa kutotoa taarifa sahihi huku wengine wakisema kuwa ni kushindwa kulizingira eneo hilo ili kuepusha ajali.

Uswidi yaitaka China kuonyesha ushirikiano katika uchunguzi kuhusu nyaya zilizokatwa katika bahari ya Baltic

g
Maelezo ya picha,Meli ya China Yi Peng Three katika mlango bahari wa Kattegat karibu na Denmark

Sweden imeiomba rasmi China kushirikiana na uchunguzi kuhusu uharibifu wa nyaya mbili katika bahari ya Baltic baada ya meli ya China kuhusishwa na matukio hayo.

Nyaya hizo, mmoja unaounganisha Uswidi na Lithuania, na mwingine ukiunganisha Ufini na Ujerumani – ziliharibiwa katika eneo la maji ya Uswidi katika Bahari ya Baltic mnamo 17 na 18 Novemba.

Meli ya China, Yi Peng Three, inaaminika kuwa katika eneo hilo wakati huo na tangu wakati huo imetia nanga katika maji ya kimataifa karibu na Denmark.

China imekanusha kuhusika na hujuma yoyote.

Watu 15 wamefariki, zaidi ya 100 hawajulikani walipo kufuatia maporomoko ya ardhi mashariki mwa Uganda

h
Maelezo ya picha,Timu ya Wanachama wa Chama cha Msalaba Mwekundu cha Uganda (URCS) wanafanya kazi kwa ushirikiano na mamlaka za mitaa na wanajamii baada ya maporomoko ya ardhi yaliyosababishwa na mvua kubwa, katika Wilaya ya Bulambuli, Uganda, Novemba 28, 2024.

Watu 15 wamefariki na wengine takriban 100 hawajulikani walipo baada ya maporomoko ya ardhi yaliyosababishwa na mvua kubwa kuzika nyumba nyingi katika vijiji kadhaa mashariki mwa Uganda, ofisi ya waziri mkuu na polisi zilisema Alhamisi.

Maporomoko ya ardhi yalitokea siku ya Jumatano katika wilaya ya Bulambuli, takriban kilomita 300 (maili 190) mashariki mwa mji mkuu Kampala.

Takriban kaya 40 zilizikwa kabisa, Chama cha Msalaba Mwekundu cha Uganda kilisema katika taarifa yake, huku zingine zikiharibiwa kwa kiasi.

“Tuna watu 15 waliokufa na hofu ni kwamba kuna miili mingi zaidi ambayo bado imezikwa,” alisema Charles Odongtho, msemaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu (OPM) ambayo inafanya kazi ya kukabiliana na majanga nje ya nchi.

Aliongeza kuwa zaidi ya watu 100 bado hawajapatikana katika vijiji vinane.

Waasi wa Syria wafanya mashambulizi makubwa kaskazini magharibi na kutwaa eneo

g
Maelezo ya picha,Waasi wa Syria wamesema walianzisha mashambulizi ili “kuzuia uchokozi” wa serikali

Majeshi ya waasi yamefanya mashambulizi makubwa kaskazini-magharibi mwa Syria, na kuyateka maeneo ya wanajeshi wa Rais Bashar al-Assad kwa mara ya kwanza baada ya miaka kadhaa.

Kundi la wapiganaji wa Kiislamu la Hayat Tahrir al-Sham (HTS) na makundi washirika yalisema yamechukua udhibiti wa miji kadhaa na vijiji katika majimbo ya Aleppo na Idlib tangu Jumatano.

Jeshi la Syria lilisema vikosi vyake vilikuwa vikikabiliana na mashambulizi “makubwa” ya “magaidi” na kuwasababishia hasara kubwa.

Kundi la waangalizi wa Syria lenye makao yake makuu nchini Uingereza limesema zaidi ya wapiganaji 180 wa pande zote mbili wameuawa katika mapigano hayo.

Takriban raia 19 pia wameuawa katika mashambulizi ya anga ya Syria na Urusi katika maeneo yanayodhibitiwa na upinzani, iliongeza.

Usitishaji mapigano umefanikiwa kwa kiasi kikubwa lakini Waisraeli karibu na mpaka wa Lebanon wana mashaka,

g
Maelezo ya picha,: Nyumba nyingi za Kiryat Shmona zimeharibiwa – wakaazi wengine wanasema kusitishwa kwa mapigano kutaurudisha mji huu tena katika hali ya maisha ya kawaida.

Israel inasema vikosi vyake vimefyatua risasi na kufanya mashambulizi ya anga dhidi ya maeneo yaliyolengwa ya kusini mwa Lebanon, katika siku ya pili ya usitishaji mapigano uliosimamiwa baada ya zaidi ya mwaka mmoja wa vita kati ya Israel na kundi la wanamgambo wa Lebanon Hezbollah.

Jeshi la Israel limesema limewafyatulia risasi washukiwa baada ya kuona shughuli katika kituo cha silaha cha Hezbollah, na magari yakiwasili katika maeneo kadhaa ambayo yalikiuka masharti ya makubaliano ya kusitisha mapigano.

Lebanon iliishutumu Israel kwa kukiuka makubaliano “mara kadhaa” na kusema inafuatilia hali hiyo.

Hadi sasa usitishaji wa mapigano unaonekana kufanikiwa kwa kiasi kikubwa, na barabara ya kijeshi ya Israeli inayoelekea ncha ya kaskazini ya mpaka wa Lebanon ilikuwa na tulivu kuliko ambavyo imekuwa kwa miezi kadhaa.

Kupitia lango lililo wazi, nilishuhudia askari walikuwa wakifanya matengenezo ya kawaida ya zana za kijeshi.

Nahodha mmoja, ambaye alivuka Lebanon asubuhi ya leo, aliniambia yeye na timu yake walikuwa na furaha kuondoka kwenye mapigano na kurejea katika maisha yao ya kawaida, lakini akisema anatumai pande zote zimetekeleza yanayohitajika.

“Lasivyo, sote tunaelewa kuwa tutajikuta tumerudi hapa hivi karibuni,” alisema.

“Binafsi, nadhani bado kuna kazi ya kufanya. Ni wazi kwamba Hezbollah bado ina nguvu za kutosha kuitishia Israel.”

kipenga cha michezo.

Tanzania yapanda kenya yashuka katika orodha mpya ya Fifa duniani

g

Timu ya taifa ya Kenya ya mpira wa miguu Harambee Stars imeshuka kwa nafasi mbili katika viwango vya hivi punde vya Fifa vilivyotolewa Alhamisi na shirikisho hilo la soka duniani.

Timu ya taifa ya kandanda sasa iko katika nafasi ya 108, chini kutoka nafasi ya 106 iliyokuwa nayo Oktoba.

Kushuka huku kumefuatia kushindwa kufuzu kwa Fainali za Mataifa ya Afrika 2025 huku Kenya ikishindwa kupata tiketi ya kushiriki michuano hiyo yenye hadhi ya juu zaidi barani.

Stars ilimaliza ya tatu katika Kundi J nyuma ya Cameroon na Zimbabwe kufuatia sare ya 1-1 dhidi ya timu ya taifa ya Namibia na sare tasa dhidi ya Namibia katika mechi mbili za mwisho za kufuzu mapema mwezi huu.

Timu hiyo pia ilitwangwa mabao 2-0 na kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Sudan Kusini katika mchezo wa awamu ya kwanza ya kuwania kufuzu ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) ingawa Kenya tayari imefuzu kushiriki michuano hiyo ikiwa ni mwenyeji pamoja na Tanzania na Uganda.

Uganda imesalia na nafasi yake ya juu zaidi katika ukanda wa Cecafa licha ya kushuka kwa nafasi moja hadi 88 huku Morocco ikisalia kuwa nchi iliyo juu zaidi barani Afrika katika nafasi ya 14.

Tanzania ilikuwa miongoni mwa nchi zilizofanya vyema katika viwango hivyo kwani iliruka nafasi sita kutoka nafasi ya 112 hadi 106, hatimaye kuipita Kenya.

Taifa Stars itaelekea Morocco mwaka 2025 baada ya kushikilia nafasi ya pili katika Kundi H baada ya kushika nafasi ya pili nyuma ya DR Congo katika mchujo.

Argentina inasalia kuwa kikosi kinachoongoza juu kwenye viwango vya FIFA, huku Ufaransa na Uhispania zikihifadhi nafasi zao katika nafasi ya pili na ya tatu mtawalia.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment