Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Saa chache baada ya ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Jean-Noël Barrot nchini Chad, waziri mwenzake Abderaman Koulamallah amechapisha taarifa kwa vyombo vya habari hivi punde siku ya Alhamisi, Novemba 28 kubaini”mwisho wa ushirikiano wa kiulinzi uliotiwa saini na Jamhuri ya Ufaransa”.

Chad inasitisha mkataba wa ushirikiano wa kiulinzi uliotiwa saini na Ufaransa, na kurekebishwa mwaka wa 2019. Bila, kwa sasa, kutoa maelezo zaidi kuhusu kusitishwa kwa mkataba huu. Tangazo hilo limetolewa sio wakati wa ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Jean-Noël Barrot ya saa 24 nchini humo, lakini saa chache baada ya kuondoka kwake.
“Serikali ya Jamhuri ya Chad inafahamisha raia wake na jumuiya ya kimataifa kuhusu uamuzi wake wa kusitisha mkataba wa ushirikiano wa kiulinzi uliotiwa saini na Jamhuri ya Ufaransa,” amesema Abderaman Koulamallah katika taarifa iliyochapishwa kwenye ukurasa rasmi wa Facebook ya wizara hiyo.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Chad anabaini kwamba Chad inataka kubadilika, lakini Ufaransa inasalia kuwa mshirika muhimu. N’Djamena inahakikisha kwamba masharti yaliyotolewa kwa ajili ya kusitishwa kwa mkataba huo, ikiwa ni pamoja na muda wa notisi, yataheshimiwa. “Serikali inapenda kusisitiza kwamba uamuzi huu hautii shaka uhusiano wa kihistoria na uhusiano wa urafiki kati ya mataifa hayo mawili,” inaongeza taarifa kwa vyombo vya habari kutoka wizara hiyo, ambayo inatarajia “mabadiliko ya usawa” na bado iko “wazi” kwa mazungumzo yenye kujenga ili kuchunguza aina mpya za ushirikiano”.

Je, kauli hii ina maana gani? Je, huku ni kuondoka kwa wanajeshi wote wa Ufaransa kutoka ardhi ya Chad? Kuna karibu wanajeshi 1,000, anakumbusha mwandishi wetu wa habari Alexandra Brangeon. Je, huu ni wito wa kutazama upya ushirikiano? Maswali ambayo hayajajibiwa kwa sasa: hakuna kilichofichuliwa kufuatia mahojiano siku hiyo hiyo kati ya Rais wa Chad Mahamat Idriss Déby na mkuu wa diplomasia ya Ufaransa Jean-Noël Barrot. Hakuna upande ulioonekana kuonyesha dalili zozote za kuzorota kwa mahusiano. Kwa upande wa Ufaransa, hakukuwa na tamko lolote siku ya Alhamisi jioni.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.