Senegal: Emmanuel Macron atambua ‘mauaji’ ya Thiaroye mnamo 1944

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Katika barua iliyotumwa kwa Rais wa Senegal hivi punde siku ya Alhamisi, Novemba 28, Emmanuel Macron anathibitisha kwamba “Ufaransa lazima itambue” kwamba kulikuwa na “mauaji” katika kambi ya kijeshi ya Thiaroye, nje kidogo ya mji wa Dakar, Desemba 1 1944. Vikosi vya mkoloni waliwafyatulia risasi wapiganaji waliokuwa wakidai kulipwa malimbikizo ya malipo yao. Idadi rasmi ya jeshi ya vifo 70 inapingwa na wanahistoria, ambao wanakadiria kuwa mamia kadhaa waliuawa.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akiwa na mwenzake wa Senegal Bassirou Diomaye Faye katika ikulu ya Élysée, Juni 20, 2024.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akiwa na mwenzake wa Senegal Bassirou Diomaye Faye katika ikulu ya Élysée, Juni 20, 2024. AP – Andre Pain

Katika mahojiano na kituo cha France 2, Rais wa Senegal Bassirou Diomaye Faye ametangaza siku ya Alhamisi, Novemba 28 kwamba Emmanuel Macron ametambua katika barua aliyomtumia “mauaji” ya wapiganaji wa Kiafrika, kitendo kilichotekelezwa na vikosi vya wakoloni wa Ufaransa katika kambi ya kijeshi ya Thiaroye, Desemba 1, 1944. Neno hilo lilitumiwa kwa mara ya kwanza katika barua rasmi, iliyoandikwa siku chache kabla ya sherehe zilizopangwa nchini Senegal, wakati ambapo Emmanuel Macron atawakilishwa na Waziri wake wa Mambo ya Nje.

Katika barua hii, rais wa Ufaransa anaandika kwamba “Ufaransa lazima itambue kwamba siku hiyo, makabiliano ya askari na wapiganaji wa kiafrika kutoka Senegal ambao walitaka malipo yao yote halali walipwe, yalianzisha mlolongo wa matukio ya ukweli uliosababisha mauaji. » Bassirou Diomaye Faye amekaribisha “hatua thabiti ambayo inapaswa kufungua mlango wa ushirikiano kwa udhihirisho wa ukweli kuhusu tukio hili la kuhuzunisha”.

Emmanuel Macron pia anabaini kazi muhimu ya wanahistoria. “Ni muhimu kujua iwezekanavyo sababu na ukweli uliosababisha janga hili,” ameandika. Rais wa Ufaransa ameomba kufahamishwa maendeleo ya kazi ya kamati iliyoundwa nchini Senegal kujua ukweli kuhusiana na tukio hili.

Mkuu wa nchi wa Senegal anaamini kwamba “hadi ukweli utakapothibitishwa kabisa” mauaji haya yatasalia “kidonda” katika historia ambayo Ufaransa na Senegal zinashiriki. Kwa sababu Senegal, kama wanahistoria wengi nchini humo, ina hakika: Ufaransa bado inaficha taarifa muhimu kuhusu mauaji haya, anakumbusha mwandishi wetu wa habari huko Dakar, Léa-Lisa Westerhoff.

Aurélien Devernoix

Miongoni mwa vipande vya kati vilivyokosekana kwenye kumbukumbu ambayo ilitolewa mwaka wa 2014 na Ufaransa, Orodha ya walioandikishwa asubuhi ya Desemba 1, lakini pia idadi kamili ya wapiganaji waliotua Dakar baada ya kuondolewa kwao, ripoti inayoonyesha mahali ambapo wapiganaji hao waliuawa, kuzikwa, au hata orodha ya waathiriwa, ni muhimu kujibu swali hili lisilojulikana la idadi kamili ya vifo.

Hati hizi zipo? Hii ndiyo changamoto nzima ya misheni ya wanahistoria na watunza kumbukumbu wa Senegal ambao kwa muda wa wiki mbili walipekua kwa undani nyaraka zilizopo. Ufaransa inasema, kuanzishwa kwa haraka kwa misheni hii ni uthibitisho kwamba haina chochote cha kuficha na kwamba imejitolea kusaidia kufichua ukweli.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment