Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Maisha ni kama mshale unaocheza katikati ya mstari WIMA (JUU) na MLALO (CHINI) na huanzia pale mistari hiyo ilipoungana.
:
Maana yake ni kwamba, maisha yana kupanda na kushuka kwa nyakati tofauti tofauti.
:
1. Kuna mda maisha yanaweza yakakunyokea mambo Yako yanaenda vizuri katika kazi, bishara, masomo n.k. Yaani, hapo mambo Yako yamesimama wima.
:
2. Kuna kipindi pia ambapo mambo yako yamebalance, yaani si mazuri Sana Wala si mabaya Sana. Hapo, mshale wako umepiga katikati ya juu na chini.
:
3. Na kipindi ambapo, mambo yanaonekana kama vile hayaendi, kila unachogusa hakisogei Wala hakifanikiwi, ambapo ni kwamba mshale uko kwenye mstari chini.
:
Kikubwa Cha kujifunza ni kwamba, maisha ni kama mshale unaocheza katikati ya JUU na CHINI Wala HAISIMAMI. Yaani, mshale ambao unaweza kuitiikia (respond) na kusogea kwa upande ambao SISI tutaweka juhudi kuifuatisha.
:
Ndiyo Kuna mda mwingi tutautumia mda mwingi Sana, juhudi kubwa, Maarifa na Ujuzi mwingi kujaribu kuipandisha mshale unyooke Wima katika mambo fulani fulani, LAKINI nafasi kubwa IPO kwamba tutafanikiwa kwa kuamua, Kuliko kukata tamaa, kuachili mshale ushuke na kulala chini kabisa.
:
Busara kubwa ni kwamba, Daima ukumbuke kuwa siku zote maisha ya Mwanadamu ni kupanda kupandisha mshale usimame wima, Lakini pia ukumbuke kuwa Siku zote zipo tu changamoto zinazoweza kukuvuta Nyuma (Pulling Back Forces) Ili uanguke chini.
:
Kikubwa ni kwamba uwezekano wa kupanda juu, kubalance au kushusha chini ipo akilini, mioyoni na mikononi mwetu.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.