Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Nchini Kenya, tangu katikati ya mwezi Novemba, Makanisa kadhaa yameeleza kutokuwa na imani na rais wa nchi hiyo na sera zake.
Nchini Kenya, makanisa yanampa kisogo William Ruto, Rais wa Kenya. Mnamo Novemba 27, 2024, Muungano wa Makanisa ya Kiinjili nchini Kenya (EAK) ulitoa wito wa Kongamano la Kitaifa la Urejesho, kujadili changamoto zinazokabili nchi. Muungano huo umezungumza kwa kukosoa utawala wa rais wa Kenya.
“Ni wakati wa Wakenya kukusanyika ili kutetea Taifa letu dhidi ya mashambulizi mengiyanayolikabili,” Askofu Philip Kitoto alisema siku ya Jumatano. Anatoa orodha pana ya ukosoajiunaoikabili sera ya William Ruto: ushuru mwingi, mageuzi yasiyofaa ya afya na elimu, ufisadi, ghasia za polisi, mashambulizi dhidi ya uwiano wa kijamii…
Kanisa la kwanza lililoanza kumkosoa rais wa Kenya ni Kongamano lenye nguvu la Maaskofu Katoliki nchini Kenya. Mnamo Novemba 14, lilimshutumu William Ruto kwa “utamaduni wa uwongo”. Lina wasiwasi kuhusu nia ya rais kusalia madarakani. Mageuzi ya kikatiba kwa kweli yanafanyiwa kazi, ili kuongeza muhula wa urais kutoka miaka mitano hadi saba.
Tangu wakati huo, Kanisa la Anglikana la Kenya, Presbyterian, Akurinos – kanisa lenye waumini 500,000 katikati mwa nchi – na Muungano wa Makanisa (skanisa la kiekumene) wamefuata mfano huo.
Katika Hotuba yake kwa taifa wiki iliyotangulia, William Ruto aliahidi kuwasikiliza viongozi wa kidini nchini. Ukosoaji unaomdhoofisha: nchini Kenya, zaidi ya 85% ya wakaazi wa nchi hiyo ni Wakristo.
Mwishoni mwa mwezi wa Juni, Rais William Ruto, ambaye aliingia mamlakani mwaka wa 2022 kwa ahadi ya kuwatetea watu walio na maisha duni, aliondoa rasimu ya bajeti iliyopingwa mitaani na vuguvugu la amani hapo awali, lakini ambalo liligeuka kuwa machafuko, haswa katika mji mkuu, Nairobi.
Mashirika ya haki za binadamu yalikashifu ukatili na, kulingana na wao, ukandamizaji usio na uwiano na haramu dhidi ya mikusanyiko hii, pamoja na vifo wakati wa makabiliano haya ya makumi ya watu na kukamatwa kiholela kwa makumi ya wengine.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.