Niger: Wapiganaji wapya zaidi ya mia moja kutoka makundi ya waasi wajisalimisha

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Takriban wanachama mia moja wa makundi mawili ya waasi nchini Niger, moja lililoundwa kumuunga mkono Rais Mohamed Bazoum aliyepinduliwa na mapinduzi ya kijeshi na kutekwa na jeshi lililo madarakani, wamejisalimisha siku ya Jumatano, Novemba 27, imetangaza redio ya serikali iliyonukuliwa na shirika la habari la AFP.

Wanajeshi wa Niger wakitembea karibu na mabaki baada ya mashambulizi ya kujitoa mhanga huko Agadez, Niger.
Wanajeshi wa Niger wakitembea karibu na mabaki baada ya mashambulizi ya kujitoa mhanga huko Agadez, Niger. © AP

“Wapiganaji zaidi ya mia moja wa chama cha Patriotic Liberation Front na Movement for Justice and Rehabilitation of Niger wameamua kuweka chini silaha zao, na hivyo kuashiria kurejea kwao kwenye uhalali,” imesema Voix du Sahel.

Sherehe iliandaliwa huko Agadez, mji mkubwa kaskazini mwa Niger karibu na Libya, wakati ambapo waasi wa zamani walikabidhi “silaha kubwa za vita” na “karibu magari kumi na tano” kwa gavana wa eneo hilo, Jenerali Ibra Boulama, radio ya serikali imesema.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment