Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Serikali ya Burundi imetangaza kuwa imewaachilia wafungwa 4,000 wanaotuhumiwa kwa “uhalifu mdogo” katika wiki za hivi karibuni ili kupunguza msongamano katika magereza yake yenye msongamano mkubwa wa wafungwa. Mpango huu uliozinduliwa katikati ya mwezi wa Novemba unalenga kuachilia jumla ya watu 5,442, ofisi ya rais imeongeza katika ujumbe uliochapishwa kwenye mtandao wa X.

Magereza kumi na moja nchini humo yenye uwezo ya kupokea kwa jumla wafungwa 4.100 , yalikuwa na wafungwa 13,211 mwishoni mwa mwezi wa Oktoba, katika mazingira yanayoelezwa kuwa “yasiyo ya kibinadamu”. Shirika la Haki za Binadamu la Ligue Iteka, moja ya mashirika kongwe zaidi ya haki za binadamu nchini Burundi, imeelezea masikitiko yake kuona hatua hii “inawaacha kando maelfu ya wafungwa wa kisiasa ambao wamefungwa magerezani.” “Wengine tayari wametumikia vifungo vyao lakini hawajaachiliwa,” amebainisha kiongozi wa shirika hilo Anschaire Nikoyagize.
Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye alitangaza maelfu ya watu walioachiliwa mnamo Novemba 14, na kuwahalalisha hasa kwa “gharama kubwa” ya wafungwa hao. “Takriban wafungwa 4,000 kati ya 5,442 tayari wamejiunga na familia zao,” ofisi ya rais imesema kwenye mtandao wa X, na kuongeza kuwa “muda wa wiki mbili kwa wale walio na jukumu la kukamilisha taratibu” umetolewa.
Mazingira ya kuwekwa kizuizini nchini Burundi mara kwa mara hushutumiwa. “Tunaweza kukaa siku kadhaa bila kuwa na chakula, hakuna dawa, wengi wa wafungwa wanalala chini, na magereza mara nyingi hayana mafuta ya kutupeleka mahakamani,” mmoja wao kwa sharti la kutokujulikana ameliambia shirika la habari la AFP.
“Tunakaribisha hatua iliyoamuliwa na rais,” alisema rais wa Chama cha Mshikamano na Wafungwa na Familia zao, Jean-Marie Nshimirimana siku ya Jumanne. “Lakini tunaona kwamba wale walio na jukumu la kutekeleza sheria hiyo wanaburuta miguu,” ameongeza,
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.