Urusi yamfukuza mwanadiplomasia, kuwaadhibu mawaziri wa Uingereza

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Mvutano unaongezeka kati ya London na Moscow, ambayo iliamua Jumanne kupiga marufuku kuingia nchini humo kwa wanasiasa wengi kutoka kwa serikali ya Keir Starmer.

Bendera ya Uingereza ikipepea mbele ya balozi wa Uingereza na kwenye gari la Urusi karibu na jengo la Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi huko Moscow, Urusi, Machi 17, 2018.
Bendera ya Uingereza ikipepea mbele ya balozi wa Uingereza na kwenye gari la Urusi karibu na jengo la Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi huko Moscow, Urusi, Machi 17, 2018. AP – Pavel Golovkin

Urusi imetangaza siku ya Jumanne kwamba imemfukuza mwanadiplomasia wa Uingereza anayetuhumiwa kwa ujasusi, jambo ambalo London imepinga vikali, na kuwawekea vikwazo karibu mawaziri kumi kutoka serikali ya Keir Starmer, sehemu mpya ya mvutano kati ya nchi hizo mbili katikati ya mzozo wa Ukraine.

Kilele hiki cha mvutano kinakuja katikati ya mzozo kati ya Urusi na nchi za Magharibi kuhusu Ukraine, baada ya London na Washington kuidhinisha Kyiv kushambulia eneo la Urusi kwa makombora kutoka Uingereza ya Storm Shadow na ATACMS kutoka Marekani.

Moscow imejibu kwa kurusha kombora la masafa ya kati – lisilo na kichwa chake cha nyuklia – kwa Ukraine na kutishia kuwashambulia washirika wa Kyiv, ambayo Uingereza ni moja ya washirika muhimu zaidi. Uhusiano kati ya Moscow na London tayari ulikuwa mbaya kabla ya mzozo, haswa baada ya kupewa sumu wapinzani wa Urusi Litvinenko (2006) na Skripal (2018).

“Shughuli za ujasusi na upelelezi”

Mwanadiplomasia aliyefukuzwa, aliyewasilishwa na idara ya ujasusi ya Urusi (FSB) kama “katibu wa pili wa idara ya kisiasa ya ubalozi wa Uingereza huko Moscow”, “alikuwa afisa w idara  ya ujasusi ya Uingereza” na “alifanya shughuli za ujasusi na upelekezi” nchini Urusi, imesema Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi.

Kulingana na FSB, iliyonukuliwa na mashirika ya habari ya Urusi, mwanadiplomasia huyu sasa ana “wiki mbili” kuondoka Urusi. Diplomasia ya Uingereza imeshutumu “madai yasiyoeleweka na yasiyo na msingi” na kuahidi jibu “kwa wakati unaofaa”.

Tishio la kulipiza kisasi

Mjini Moscow, balozi wa Uingereza, Nigel Casey, ameitwa katika Wizara ya Mambo ya Nje siku ya Jumanne. Katika mchakato huo, diplomasia ya Urusi imetangaza kuwa itapiga marufuku mawaziri wengi wa Uingereza kuingia Urusi, ikiwasilisha uamuzi huu kama jibu kwa sera za London kwa wanasiasa “wanaozungumza Kirusi”.

Orodha hiyo inajumuisha Waziri wa Fedha Rachel Reeves, Naibu Waziri Mkuu Angela Rayner, Waziri wa Mambo ya Ndani Yvette Cooper na zaidi ya dazeni ya wanasiasa wengine wakuu kutoka serikali ya Leba ya Keir Starmer.

“Moscow haitavumilia shughuli za maafisa wa ujasusi wa Uingereza ambao hawajatangazwa katika eneo la Urusi,” wanadiplomasia wake wamehakikisha, na kuahidi “jibu sawa katika kulipiza kisasi (…) ikiwa London itazidisha hali hiyo.”

Muingereza akamatwa

Mapema siku ya Jumanne, mahakama ya Urusi ilithibitisha, baada ya kusikilizwa kwa kesi iliyofanyika kwa faragha, kwamba ilikuwa imemweka rumande James Anderson, Muingereza anayeshutumiwa kwa kulipigania jeshi la Ukraine katika eneo la Kursk la Urusi, ambapo Kyiv ilianzisha mashambulizi ya kuvuka mpaka mwezi Agosti.

Mamlaka inamshutumu James Anderson, 22 kuvuka mpaka wa Urusi “kinyume cha sheria” kabla ya kushiriki katika “vita” katika eneo la Kursk kwa niaba ya jeshi la Ukraine.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment