Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Mkuu wa Baraza Kuu la Sudani, Jenerali Abdelfattah Al-Burhan, amefanya ziara rasmi katika nchi jirani ya Eritrea siku ya Jumanne, Novemba 26. Majadiliano yamefanyika katika ikulu ya rais ili, kulingana na taarifa kwa vyombo vya habari kutoka Baraza Kuu la Sudan, “kuunganisha uhusiano wa pande mbili na wa kihistoria” kati ya nchi hizo mbili.

Jenerali Abdel Fattah Al-Burhan alifanya ziara rasmi katika nchi jirani ya Eritrea siku ya Jumanne, Novemba 26: ameandamana na mkuu wa upelelezi pamoja na Waziri wa Utamaduni na Habari. Rais Isaias Afwerki alikuja kukutana nao katika uwanja wa ndege wa Asmara.
Eritrea inaunga mkono jeshi la serikali na ni katika ardhi yake ambapo vikosi vinavyounga mkono jeshi dhidi ya Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) vinafanya mazoezi. Wizara ya Mambo ya Nje ya Eritrea imekashifu mara kwa mara uhalifu wa RSF unaofanywa nchini Sudani tangu kuanza kwa vita. Nchi hii pia inapokea maelfu ya wakimbizi wa Sudani.
Eneo la mpaka lililodhibitiwa na FSR
Jenerali Al-Burhan alitoa shukrani zake kwa jukumu hili la Asmara. Ana nia ya kuunganisha muungano huu ambao unamuwezesha kukabiliana na washirika wa kikanda wa FSR. Ama kuhusu Asmara, ambayo inashiriki kilomita 600 za mpaka na Sudani, inaweza kuhakikishiwa zaidi kuhusu usalama wa mpaka wake.
Muda wa ziara hii sio mdogo. Inakuja siku chache baada ya kutekwa tena na jeshi la serikali Sinja, mji mkuu wa jimbo la Sannar, linalopakana na Eritrea. Kwa mujibu wa waangalizi kadhaa, haya ni mafanikio ya kimkakati ambayo yatawezesha jeshi kutwaa tena maeneo ya mashariki na katikati mwa Sudani ili kusonga mbele kuelekea jimbo la Al-Jazirah na kuwadhibiti wanamgambo wa RSF.
Siku ya Jumatatu, Jenerali Al-Burhan alipaza sauti yake tena, akikataa majadiliano yoyote mapya na RSF kabla hawajaweka silaha zao chini. “Familia ya wahalifu ya Dagalo itapondwa,” amesema, na hivyo kufunga uwezekano wowote wa majadiliano.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.