Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Thobias Makoba akizungumza na waandishi wa habari./Picha: @TZMsemajiMkuu
Idadi ya watu waliopoteza maisha katika tukio la kuporomoka jengo nchini Tanzania, sasa imefikia 29, serikali ya nchi hiyo imesema.
Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania Thobias Makoba, amesema kuwa shughuli nzima ya uokoaji katika eneo la soko la Kariakoo, imekamilika siku ya Novemba 26, huku idadi ya vifo vinavyotokana na tukio hilo la Novemba 16 ikifikia 29.
Hii ni baada ya kupatikana kwa miili mingine tisa, wakati wa zoezi la uokozi likiendelea, serikali hiyo imesisitiza.
“Kuanzia Novemba 26, eneo lote la Kariakoo linafunguliwa huku shughuli mbalimbali zikiendelea…isipokuwa eneo moja tu lililohusisha ghorofa kuporomoka ndilo litaendelea kufungwa kwa siku tatu kwa ajili ya kumalizia zoezi la uchunguzi,” alisema Makoba.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.