Msumbiji: TotalEnergies inajua kuhusu ukiukaji wa haki za binadamu Cabo Delgado

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Miezi miwili iliyopita, vyombo vya habari vya mtandaoni Politico viliripoti kuwa mwaka wa 2021 nchini Msumbiji jeshi liliteka nyara, kubaka na kuwaua raia katika makontena yaliyokuwa kwenye mlango wa eneo lililowekwa kwa ajili ya mradi wa gesi wa TotalEnergies.

Kikosi cha wanamaji wa Msumbiji wanaonekana kwenye gati za kiwanda cha gesi cha Total LNG huko Afungi, katika jimbo la Cabo Delgado, Msumbiji, Septemba 29, 2022.
Kikosi cha wanamaji wa Msumbiji wanaonekana kwenye gati za kiwanda cha gesi cha Total LNG huko Afungi, katika jimbo la Cabo Delgado, Msumbiji, Septemba 29, 2022. AFP – CAMILLE LAFFONT

Kampuni ya mafuta ya Ufaransa ilikanusha kuwahi kupokea habari kwamba matukio kama hayo yalikuwa yamefanyika. Lakini kampuni hii ya mafuta ya Ufaransa ilijua habari hii, kulingana na hati za ndani za kampuni hiyo zilizopatikana na Gazeti la kila siku la Le Monde.

Kwa mujibu wa nyaraka za ndani za kampuni ya mafuta ya Ufaransa, zilizopatikana na Gazeti la kila siku la Le Monde, TotalEnergies ilifahamu – kuanzia mwaka 2021 – kuhusu ghasia za mara kwa mara ambazo vikosi vya usalama vya Msumbiji viliwasababishia raia katika eneo jirani. Hii inathibitishwa na ripoti za robo mwaka za kijamii za kampuni yake tanzu nchini Msumbiji LNG. Katika hati hizi za siri zilizokusudiwa kwa idara ya Mikopo ya Mauzo ya Nje ya Italia, imeandikwa kwamba “tangu Aprili 2, 2021, wakazi wameripoti mara kwa mara ukiukaji wa haki za binadamu unaofanywa na Kikosi Kazi cha Pamoja, (Joint Task Force)”, jeshi la Msumbiji na polisi wanaolipwa kulinda eneo la gesi.

Marupurupu ya askari hawa pia yamesimamishwa kwa miezi miwili, kulingana na waraka huu. Katika ripoti iliyofuata, kampuni tanzu ya TotalEnergies inaibua hatima ya wavuvi wawili, waliopigwa na vikosi hivi vya usalama, mmoja wao aliuawa, mnamo mwezi Machi 2022.

Kampuni ya mafuta ya Ufaransa inaweka mbele “mazingira duni ya usalama”

Idara ya mawasiliano ya TotalEnergies, ambayo imeombwa kujieleza, leo inataja “mazingira duni ya usalama” wakati huo ambayo “yalisababisha kuongezeka kwa hatari” ya unyanyasaji, kitedo ambacho kampuni ya mafuta ya Ufaransa ilijaribu kujilinda kupitia mafunzo ya kijeshi, motisha ya kifedha na mfumo wa malalamiko na uchunguzi.

TotalEnergies, tangu ripoti ya mwanadiplomasia Jean-Christophe Rufin mnamo mwezi Machi 2023, ilivunja makubaliano yake na Kikosi Kazi hiki cha Pamoja, Joint Task Force.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment