HAUKO MTUPU, ‘You Are Not Empty”. Embu jifanyie Personality Check…

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Kwa haraka haraka unaweza ukasema upo kundi Namba Ngapi??

1. KIPAJI TU.

Maana yake kwa sasa unaishi kwa kutegemea KIPAJI chako tu ulichozaliwa nacho. Mf. Uchoraji, Uimbaji n.k…

2. TAALUMA TU.

Maana yake kwa sasa unaishi kwa kutegemea TAALUMA yako tu uliyosomea na kutunikiwa cheti rasmi. Mf. Ualimu, Uanasheria n.k…

3. UJUZI TU.

Maana yake kwa sasa unaishi kwa kutegemea UJUZI fulani ambayo umejifunza mwenyewe. Mf. Copywriting, Ujuzi wa Biashara fulani,…n.k.

4. KIPAJI + UJUZI.

Hapa unatumia KIPAJI chako pamoja na UJUZI ambayo ni nyenzo ya KUNOA kipaji chako.

Yaani, umeamua kuongeza wigo kwa kujifunza UJUZI fulani Ili kuboresha Kipaji chako zaidi…na kujiongezea KIPATO.

Mfano! Una Kipaji cha UANDISHI basi Unaamua kujifunza Ujuzi wa COPYWRITING Ili kujiingizia kipato zaidi

5. KIPAJI + TAALUMA.

Hapa umeoanisha KIPAJI chako na TAALUMA yako. Yaani, unajiribu ku-match kile ulichokisomea pamoja na Kipaji chako ili uweze kuwa na IMPACT kubwa zaidi.

Mfano. Una KIPAJI cha UANDISHI, alafu umesomea UDAKTARI basi ukaamua kutumia Kipaji chako kuandika Vitabu, makala za kilipwa juu ya Afya.

6. TAALUMA + UJUZI.

Hapa una kitu chako ulisomea ‘Professionally’, Lakini umejiongeza zaidi kwa KUJINOA na Ujuzi sahihi zenye kukufanya uzidi kuwa bora katika TAALUMA yako.

Mfano. Umesomea ‘Accounts and Finance’ Lakini ukaamua kujifunza ujuzi wa Sanaa ya uneni (Public Speaking) ili uweze kuwashawishi watu na kufanya kazi ya Ushauri wa kitaamu (Consultancy) kwa wajasiriamali na biashara nje ya kazi ajira yako.

7. KIPAJI + TAALUMA + UJUZI

N.B. Watu wachache sana wapo kundi hili LAKINI hapa maana yake unaamua kuwa ‘MASTERMIND’

Yaani, unapiga kote kote…

Unachanganya Kipaji chako, Taaluma yako na Ujuzi fulani fulani na kuzipika ndani ya chungu kimoja. Hapa utakuwa umeiva kote kote…unakuwa mtu ambaye sio wa kawaida kwa sababu ya umahiri wako juu ya kitu fulani.

Mfano. Una Kipaji cha Uandishi + profession ya ‘Marketing’ baadaye ukaamua kujifunza Ujuzi wa ‘Copywriting’ ili kusaidia wajasiriamali kuuza bidhaa zao zaidi kwa njia ya maandishi Mtandaoni.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment