Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Moja ya ukweli mchungu kwenye maisha ni kuwa, kila Shujaa kuna watu ambao hawamkubali.
Yaani, hata wewe uwe Mwema kiasi gani na ufanye mazuri kiasi gani, bado watakuwepo watu wanaokukosoa au kukusema vibaya.
Mbaya zaidi, watakaokuwa wanafanya hivi ni watu wako wa karibu sana.
Watu wengi wema, wamekatishwa tamaa na watu wao wa karibu. Kuna watu wamejinyima sana ili kupambania familia zao, Ila wameishia kusemwa vibaya.
Wapo watu ambao wamejitoa sana kwa wapenzi wao, Ila wameishia kuchafuliwa sifa zao.
Ni kweli inakatisha tamaa ila isibadili dhamira yako ya kuwa mwema. Ukumbuke kuwa, watu wengi wanaokusema vibaya ni aidha unachofanya hakiwagusi kabisa na hawakihitaji au ni njia ya kuonesha kuwa wana wivu mbaya.
Vyovyote itakavyokuwa, usiache Kutenda mema. Utavuna kwa wakati.
Kama umeipenda makala hii……
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.