Jordani: Mtu apigwa risasi na kuuawa baada ya risasi kusikika karibu na ubalozi wa Israel Amman

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Tukio hilo limetokea siku ya Jumapili, Novemba 24 karibu na ubalozi wa Israel mjini Amman, ambapo kijana mmoja aliwafyatulia risasi maafisa wa polisi wa Jordani.

Magari ya polisi kwenye barabara karibu na ubalozi wa Israeli huko Amman, Jordani, Novemba 24, 2024.
Magari ya polisi kwenye barabara karibu na ubalozi wa Israeli huko Amman, Jordani, Novemba 24, 2024. REUTERS – Jehad Shelbak

Kijana mwenye umri wa miaka zaidi ya ishirini aliwafyatulia risasi maafisa wa polisi wa Jordani karibu na ubalozi wa Israel mjini Amman. Shambulio hilo lilipelekea maafisa wa polisi watatu kujeruhiwa. Mshambuliaji, mwenye umri wa miaka 24, aliuawa papo hapo.

Polisi wa Jordani hawajatoa taarifa kuhusu uwezekano wa kuwa na uhusiano na makundi ya kigaidi.

Kulingana na mtaalam wa usalama Omar Al-Raddad, inaonekana kwamba shambulio hilo lilikuwa kitendo cha kipekee, kisicho na uhusiano wowote na makundi yenye silaha: “Shambulio hili lina vipengele viwili: kunaweza kuwa na uhusiano na makundi ya wafuasi wa Hamas na Hezbollah, au kunaweza kuwa na sababu za kulipiza kisasi dhidi ya polisi. Lakini ni uchunguzi ambao utalazimika kubainisha sababu.”

Shambulio lililoelezewa kama la “kigaidi”

Msemaji wa serikali Mohammed Momani ameliita shambulizi hilo la “gaidi” na kuahidi kwamba waliohusika wataadhibiwa: “Hali ya afya ya maafisa wa polisi waliojeruhiwa katika shambulio hilo iko shwari, na tunatumai watapona haraka. Kama serikali, tunawaunga mkono kikamilifu, walipokuwa wakitekeleza wajibu wao wa kulinda usalama na utulivu wa Jordani.”

Kwa zaidi ya mwaka mmoja, maandamano yamekuwa yakifanyika karibu na ubalozi wa Israel, kuunga mkono Wapalestina na kupinga vita huko Gaza. Hakuna mfanyakazi hata mmoja katika ubalozi huo , baada ya Jordani kukataa kumruhusu mwanadiplomasia wa Israel kurudi Amman.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment