Chuma Hunoa Chuma-Nukuu 10 zake Hayati Mwl Julius Nyerere.

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

1. Hakuna umaskini mbaya kama umaskini wa mawazo. Ni umaskini mbaya Sana.

2. Hatuwezi kutatua matatizo yetu kwa kujidanganya kuwa hayapo.

3. Kila anataka maendeleo, Lakini s kila mtu anaelewa na kukubali majitaji ya msingi kwa ajili ya maendeleo. Jambo kubwa ni kufanya kazi kwa JUHUDI.

4. Elimu yeyote iwe ya darasani au si ya darasani ina shabaha yake. Shabaha yenye ni kurithisha kutoka kizazi kimoja hadi kizazi kingine, maarifa na mila za taifa, nakuwaandaa vijana wawe tayari kuchukua nafasi zao katika kulitumikia na kuliendeleza Taifa. Hivi Ndivyo ilivyo katika nchi zote.

5. Njia pekee ambayo uongozi unaweza kutunzwa kama uongozi wa watu, ni pale ambapo Viongozi wanapokuwa na sababu ya kuogopa hukumu kutoka kwa watu.

6. Utii ukizidi unakuwa UOGA. Uoga huzaa unafiki na kujipendekeza, Mwisho wake ni MAUTI.

7. Watu walio hatari Sana ni wale ambao wanafikiri kuwa wanajua kila kitu, Wala hawana Cha kujifunza zaidi. Hii ni tabia mbaya ambayo huzuia kabisa maendeleo.

8. Kujielimisha ni kutafuta ukweli wa mambo.

9. Ukweli una tabia moja nzuri Sana. Haujali mkubwa Wala mdogo; haujali adui Wala rafiki. Kwake watu wote ni sawa.

10. Itakuwa ni Kosa na Haina umuhimu kudhani kuwa ni lazima tusubiri hadi Viongozi wafariki kabla ya kuunza kuwakosoa.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment