Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania Freeman Mbowe amekamatwa siku ya Ijumaa Oktoba 22, 2024 pamoja na viongozi wengine siku chache kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa nchini humo, kwa mujibu wa chama chake cha CHADEMA.
“Polisi wamevizia msafara katika msitu wa Halungu” magharibi mwa nchi “na kumkamata kiogozi wa chama, Freeman Mbowe, pamoja na viongozi wengine kadhaa walioambatana naye,” John Mrema, msemaji wa chama amesema katika mtandao wa kijamii wa X. “Polisi waliwachukua viongozi wetu bila kutaja wanakokwenda, na bado hatujui wanashikiliwa wapi au kwa sababu gani,” ameongeza, akitaka waachiliwe.
Bw. Mbowe alikamatwa kwa muda mfupi mwishoni mwa mwezi wa Septemba pamoja na makumi ya watu wakati polisi wa Tanzania walipozuia maandamano ya chama chao jijini Dar es Salaam. Tanzania imekumbwa na kukithiri kwa ukandamizaji wa kisiasa katika miezi ya hivi karibuni.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinavituhumu vyombo vya ulinzi na usalama kuhusika na upotevu wa wanachama wake kadhaa na katika mauaji ya Ali Mohamed Kibao, mmoja wa viongozi wake aliyekutwa amefariki Septemba 7. Afisa wa chama amesema alitekwa nyara na kuteswa mwezi uliopita na watu waliojitambulisha kama maafisa.
Uchaguzi wa Novemba 27 katika miji na vijiji kote nchini unatarajiwa kuwa kipimo cha hali ya kisiasa kabla ya uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika mwezi wa Oktoba 2025. Utakuwa kipimo cha kwanza kwa Rais Samia Suluhu Hassan, aliyeingia madarakani kufuatia kifo cha ghafla cha mtangulizi wake John Magufuli mwezi Machi 2021.
Rais Suluhu Hassan alionyesha dalili za uwazi wa kidemokrasia alipoingia mamlakani mnamo mwezi Machi 2021, kwa kufungua tena haraka, kwa mfano, vyombo vya habari vilivyopigwa marufuku. Lakini rais amekabiliwa na ukosoaji mkubwa katika miezi ya hivi karibuni, akishutumiwa kwa kurejea katika mazoea ya kimabavu ya mtangulizi wake katika maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa mwezi Novemba na uchaguzi mkuu mwishoni mwa mwaa 2025.
CHADEMA ilipinga mbele ya waandishi wa habari siku ya Jumanne kuenguliwa kwa “isivyo haki” kwa wagombea wake kadhaa.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.