Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Jana wakati nasoma, “Article” moja juu ya maisha ya Mfalme Sulemani, nilikutana na hili somo juu mbinu zilizomsaidia kufanikiwa katika Ujasiriamali, Biashara na Uwekezaji.
Wote tunajua kuwa Mfalme Sulemani anasadikika kuwa ni Miongoni mwa watu waliowahi kufanikiwa kuwa na utajiri mkubwa Sana.
Inasemekana katika makadirio ya sasa utajiri wake ungekuwa na thamani karibia Trilioni 2.
Ndiyo ile TRILIONI yenye “T”.
Vile vile Mfalme Sulemani anaaminika kuwa ndiye mtu mwenye Hekima na Busara nyingi kuwahi kuishi duniani.
Kwa undani zaidi unaweza kusoma Biblia au kitabu cha, “The Richest Man Who Ever Loved – King Solomon’s Secrets to Success, Wealth and Happiness”, cha STEVE SCOTT ambapo amechambua Kwa kina na tafiti zaidi.
Ila kwa sasa tupate nasaha chache kutoka kwake.
1. MUNGU KWANZA.
Mungu Kwanza, ni kauli ambayo imezoeleka Sana lakini ina Nguvu kubwa Sana. Mfalme alimtanguliza Mungu Kwa kila jambo.
MHUBIRI 5:10, “Apendaye fedha hatatosheka na fedha, wala atamaniye mali hata akiipata hatatosheka. Hilo ni bure kabisa”.
2. TAFUTA MAARIFA.
Katika unachokifanya tafuta maarifa na taarifa sahihi.
MITH 24:5, “Mtu mwenye hekima ana Nguvu; Naam, mtu wa Maarifa huongeza uwezo”.
3.BIDII
MITHALI 10:4, “Atendaye mambo Kwa mkono mlegevu huwa maskini, Bali mkono wake aliye na bidii hutajirisha”.
Weka Bidii, Bidii na Mungu atakubariki.
4. KUTOA – GIVING.
Mithali 11: 24, “Kuna mtu atoaye kwa ukarimu, hata hivyo hupata zaidi. Kuna mwingine huzuia, lakini huwa maskini”.
Toa kwa Mungu, Saidia Wahitaji.
5. EPUKA MADENI YALIYOKITHIRI.
Ni kweli madeni hayaepukiki LAKINI, ni Manageable. Mfalme anasema, tupunguze kukopa.
MITH 22:7, “Akopaye ni mtumwa wa akopeshaye”.
6. TAFUTA SHAURI NJEMA.
Mfalme anahimiza kutafuta shauri kutoka kwa watu waliofanikiwa,
MITH 3:18, “Mipango hushindwa Kufanikiwa kwa sababu ya kukosa Ushauri, bali kukiwa na washauri wengi hufanikiwa”.
7. FANYA KAZI.
Hata Wana kitaa husema, “Kazi Kazi”.
MITH 4:23, “Katika kila Kazi mna faida; Bali Maneno ya mdomo ni hasara tu”.
8.TIMING
MITH 4:5, “Mvivu halimi kwa majira; kwa hiyo wakati wa mavuno hutazama lakini hapati chochote.
Kama umejifunza kitu katika somo basi,….
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.