Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Ushawahi kujihisi unachokuliwa poa au unadharauliwa na mtu au watu fulani.
YES, zipo ishara na dalili ambazo ukiziona utahisi kuwa ulipo watu wanakuchukulia poa Sana.
Utafiti uliofanywa na Jarida la Havard Business Review (HBR) Kwa zaidi ya watu 20,000 umebainisha kuwa zaidi ya 50% ya watu hupitia katika Hali hiyo ya kujihisi kuchukuliwa poa.
NA, zifuatazo ni sababu zinazomfanya mtu kujihisi kuchukuliwa poa.
1. Kuwa na Mashaka Juu yako Binafsi.
-Hali ya kujishuku na kujihisi umuhimu wako hauonekani ni sababu kubwa uinayoweza kukufanya ujihisi kwamba unachokuliwa poa.
2. Kujiona duni katikati ya Watu waliokuzidi Uwezo na Uzoefu.
-Utafiti umebainisha kuwa unapokuwa kwenye timu ya watu waliokuzidi Uwezo kielimu, ki-ujuzi au kwa uzoefu ni rahisi sana kujidunisha na kuhisi pengine Wewe huna mchango wowote.
3. Kujishikiza tu bila kuonyesha thamani.
-Ukweli ni kwamba popote pale ulipo lazima uonyeshe thamani YAKO. Hata kama kazi yako ni ya kufanya usafi katika ofisi X.
Fanya usafi kiasi kwamba mtu akiona anasema, YES hapa kuna mtu.
Ukijishikiza sehemu kama vile upo au haupo ni rahisi kuhisi kwamba unachukuliwa poa na ni kweli utachukuliwa poa.
4. Kutoishi Kauli zako.
-Iwe katika kazi au biashara jitahidi kuweka ahadi na miadi na kutekeleza kwa wakati.
Iwe kama ikishindikana basi kwa dharura isiyokwepeka.
Pia wajulishe watu mapema kama ukihairisha.
La sivyo, ukiwa mtu wa mzaha na utani hawatakuchukulia, “SERIOUS’….Mwishowe utajihisi unachokuliwa poa.
5. Kutokuwa na Mipaka.
Usipokuwa na mipaka wala kuziheshimu basi ni rahisi sana kuchukuliwa poa.
Lazima uwe na “VALUES” ili uweze kutoa VALUE.
6. Kutokujiamini katika unachokijua.
Maji hufuata mkondo.
Ndivyo ilivyo katika Maisha ya kawaida, watu hukuchukulia vile unavyojichukulia.
Kama hujiamini katika unachokifanya siyo rahisi mtu mwingine kukuamini.
Huenda ulipo unajihisi unachokuliwa poa Kwa sababu tu umeshindwa KUJIAMINI na kuonyesha kuwa unaweza.
7. You are Too Much Available.
Kila sehemu upo.
Kila tukio upo.
Haimanishi kuwa usishiriki na kujumuika na watu wengine katika matukio mbalimbali LAKINI haimanishi uwepo katika kila mahali
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.