Unapanda cheo,ufanye vipi.

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Nilishutuka sana Jana rafiki yangu mmoja alivyonipigia simu akaniambia,..

“Edwin, I have to step out Kaka, Maisha yangu ni muhimu kuliko hiki cheo”.

YES, ilinigusa sana Kwa sababu ni miezi michache ilipita baada ya kuwa, “Promoted” kazini kuwa ‘Manager’ na tulimpongeza na kusherekea.

Na, kama rafiki yetu, tunapenda azidi kupiga hatua na wala siyo kurudi nyuma.

LAKINI, kwa upande wake kiti cha uongozi kimekuwa cha moto, “He Need a Breath”.

Nilijua pengine labda anachoka sana kwa sababu ya u-busy na majukumu mengi kumbe, LA HASHA!!

“Ameyakanyaga”…”Kiti hicho kilikuwa kinawindwa na watu wengi”. Kila mtu alikuwa anakodelea macho kuwa “Manager”.

Mbaya zaidi ni kwamba, yeye aliajiriwa hapo miaka mitatu iliyopita kama ‘Sales Representative’ baadaye akawa ‘Sales Manager’ na majuzi akawa ‘General Manager’ ‘The Boss’ wakati kuna watu waliajiriwa miaka zaidi ya 10 tangu kampuni inaanzishwa.

Pia, yeye ana shahada tu ya, “Sales and Marketing” wakati kuna Staff wenzake Wana ‘Masters’ ya ‘MBA, PSPA n.k.

Kwa hiyo kila akijiweka kwenye viatu vya wakongwe kazini “IN TERMS OF” Elimu na Uzoefu havimtoshi, na hii inamfanya sana awe “INFERIOR”.

PLUS, Maneno ya kejeli na dharau kutoka Kwa wakongwe kazini,

Wewe kijana umekuja tu juzi unataka kutusumbua?

Wewe si unapendwa Sana na Bodi Management?

Hiyo nafasi ina wenyewe dogo, muda siyo mrefu utaachia.

Kuna watu wamekuwepo tangu kampuni inaanzishwa na wamekuzidi kila kitu (elimu na uzoefu), Kwa hiyo wewe ni kivuli tu hapo?

Yes, Nilimsikiliza sana, malalamiko ya Broo na vitu vinavyomkera kazini mpaka anataka kuachia ngazi, nikagundua..!

Ni maneno ya watu tu yanayomkera, na pia anajiona pengine yeye ni mdogo kwa sasa kuwa G.M.?

Nilimuuliza swali moja, “Broo kwani wewe unahisi umechaguliwa na Bodi ya Wakurugenzi kwa sababu gani?

Akaniambia, miaka miwili tangu awe Sales Manager, “Kampuni imeingiza faida mara tatu zaidi ya miaka 5 iliyopita”.

Kwa hiyo yeye anahisi ni Ufanisi tu ndiyo inambeba, “Only Performance”.

Nikamwambia hata Mimi ningekuwa Mkurugenzi wa hiyo ningekuchagua Kaka 

Nikaendelea…”Kwa Sababu kwa miaka 2 umeongoza vizuri timu yako ya mauzo na masoko mpaka mkaingiza faida kubwa, kwa hiyo una Leadership Skills pia, ndiyo maana ukapewa hiyo nafasi”.

Na uzuri ni kwamba hiyo kampuni, ni tawi la kampuni kubwa ya kimataifa kutoka UK. Wakurugenzi wako nje, mara chache Sana wanakuja Bongo kufanya, “Monitoring and Evaluation”.

Kwa hiyo wanapima performance kwa kuangalia, “Reports, Outcome, and Impact”, Ndiyo maana zali likamdondokea jamaa, maana ameweka juhudi yake katika idara ya mauzo mpaka akawa ‘Promoted’.

LAKINI, yuko “Worried” Sana na cheo kikubwa,…”Bora nirudi Sales tu Kaka” hiyo kauli anapenda kuisema Sana kila nikiongea naye.

Mimi nilimkatalia na sikumuunga mkono katika mawazo yake ya kuachia ngazi.

Nilimshauri, wewe tenda haki, usimwonee wala kumpendelea mtu. Fuata taratibu.

“Just Be a Good Leader”.

“Wewe ungemshauri NINI huyu Kaaka?”.

Tuandikie tujifunze 

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024

.


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment