MAMBO 2 Ya KUEPUKA Ili UWE Na SIKU Ya MAFANIKIO…

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

i. Kuruhusu Habari Mbaya
ii. Kuanza Siku Kwa Malalamiko.

Leo katika makala hii tutaangalia jambo la kwanza.

– Kuruhusu Habari Mbaya

Jambo la kwanza ambalo wanaliepuka ni kuruhusu habari mbaya ambazo zinaweza kuwaharibia siku yao.

Habari hizi zinaweza kuja kwa njia ya kusikia, kusoma au kuangalia.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na mtaalamu kutoka Chuo Kikuu cha Sussex, Graham Davey na kuchapishwa kwenye jarida la Saikolojia la Uingereza ilionyesha kuwa…

…dakika 14 za habari mbaya ambazo unazipata kila siku zinaweza kukufanya uwe mtu mwenye wasiwasi kila wakati .

Katika utafiti huu ilionesha kuwa mtu ambaye
anasikiliza habari mbaya asubuhi huwa kwenye uwezekano mkubwa wa kuona kuwa…

…matatizo yake ni makubwa na hayawezekani kuliko yule ambaye hasikilizi habari mbaya asubuhi.

Unachotakiwa kujua ni kuwa hauhitaji kutumia nguvu kubwa sana kusikia…

…au kuona habari mbaya, huwa zinakuja zenyewe.

Kwa mujibu wa mtandao wa Quora, inaonesha kuwa takribani 90% ya habari unazozisikia kila siku kutoka kwenye vyanzo mbalimbali huwa ni habari hasi.

Hivyo ni lazima uamue kutumia nguvu kubwa ili kuziepuka habari hasi ili uwe salama.

Mara unapoamka asubuhi, chagua kwa makusudi kuanza kusikiliza, kusoma na kuangalia habari chanya.

Habari ambazo zitakusaidia kupata nguvu na hamasa ya kufanikiwa katika malengo yako ya siku husika.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment