Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

“Na alipokuwa katika UCHUNGU MKUBWA, akaomba kwa bidii zaidi na JASHO lake likawa kama MATONE YA DAMU ikidondoka ardhini. 45 Baada ya KUOMBA, akawarudia wanafunzi wake akawakuta WAMELALA, wamechoka kwa huzuni. (Luka 22:44-45)
Imagine, Yesu yuko kwenye Kipindi KIGUMU cha maisha Yake. Anaamua kuchukua WATU WAKE WA KARIBU ZAIDI (Wanafunzi wake), anaenda nao mahali pa Siri akiamini watasimama naye katika wakati huo.
Nini kinatokea ? Wakati yeye akiwa anatoka JASHO LA DAMU na AKIWA na UCHUNGU mkubwa, wale ambao ndio alıona watu wake wa karibu walikuwa WAMELALA.
Yaani, ni hivi: Kuna nyakati kwenye maisha yako, utatamani watu wako wa KARIBU “wafeel” maumivu yako, Ila utashangaa ndio kwanza wanaendelea na maisha yao ya kawaida.
Kuna wakati utawashirikisha, utakaa nao vikao n.k Ila mkiachana na wao wataendelea na maisha yao, hawatakumbuka hata kidogo machungu yako.
Kiufupi ni kuwa, kwenye MALENGO na MAONO makubwa ya maisha yako, Itakulazimu kukubali zile siku za KUBAKIA PEKE YAKO. Ndio; JASHO, DAMU na MAUMIVU yatakukuta.
Usiwalaumu wakiwa KIMYA/WAMELALA, wao hawahisi kile unachohisi.
USIACHE KUPAMBANIA NDOTO YAKO.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.