Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Hauhitaji kugongewa mhuri na mtu ili kuishi Ndoto yako. Mungu aliyekuumba na kuruhusu MAONO hayo ndani yako, amekupa uwezo wa KUYAFIKIA.
Tafuta ushauri Kwa watu LAKINI siyo Uthibitisho, “APPROVAL”.
Hakuna mtu ambaye amewahi kufanya kitu kunyoosha mstari kwa rula.
Kila mtu aliyefanikiwa amepitia mchakato wa kujaribu, kukosea, kupatia, kuanguka, kusimama, mpaka kutoboa.
Hivyo, punguza kutafuta uthibitisho sana wakati unataka kufanya jambo.
Itakuchelewesha sana.
Itakufanya ushindwe kujiamini.
Itakufanya uwe na hofu ya kufeli kwa kuogopa watu watakuonaje.
Itakufanya ufanye jambo Kwa ajili ya kuwaonyesha na kuwaridhisha watu na siyo nafsi yako.
Itakuchelewesha kufanya maamuzi kwa katika jambo husika.
Unawezaje kupugunza kutafuta, “VALIDATION”.
1. Amini katika uwezo wako.
2. Shirikisha watu wachache unaowamini jambo lako, kisha pokea Mawazo yao kama Ushauri na kuchuja.
3. Uwe mtu wa mwisho katika kuamua.
4. Uwe na MENTOR katika eneo hilo,,,,”Awe tu, anaku-GUIDE na siyo kukuamulia”.
5. Uwe na Utayari wa kujaribu vitu vipya, hata kama hakuna mtu aliyewahi kufanya katika, “Circle yako”.
6. Tafuta taarifa ya kutosha juu ya jambo husika ili uweze kujua “IN and OUT” ya jambo husika.
7. Usitafute kuwa, “PERFECT”… Jitahidi ku-FOCUS katika IMPROVEMENT yaani kufanya kwa kuboresha kila siku.
8. Amini katika mchakato, kwamba hata watu 1000 wakikudhibitisha,, bado Tu utapitia katika mchakato Fulani mapka ufanikishe jambo husika.
9. Uwe wa kwanza kujutia Moyo na uwe wa mwisho kujikatia tamaa. Ndoto ni YAKO,, Maisha ni yako.
10. Mwamini MUNGU aliyekupa MAONO hayo. Yakabidhi kwake,,kisha weka NIA, JUHUDI na MAOMBI.
Hakuna lisilowezekana kwake.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.