Uingereza yatangaza vikwazo kwa mamluki wanaohusishiwa na Urusi

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Serikali ya Uingereza imetangaza vikwazo kwa kampuni tatu binafsi za ulinzi zinazofanya kazi zake barani Afrika kwa ushirikiano na serikali ya Urusi na kundi la mamluki la Wagner

Mamluki wa Wagner wakiwa kaskazini mwa Mali.
Mamluki wa Wagner wakiwa kaskazini mwa Mali. AP

Vikwazo hivyo, hivyo vitaathiri kampuni hizo ikiwemo Africa Corps, ambayo imechukua nafasi ya Wagner barani Afrika kwa kuendeleza shughuli zake nchini LibyaMali na Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Uingereza inasema vikwazo hivyo vinalenga kuzuia uovu na shughui haramu zinazoendelezwa na kampuni hayo katika mataifa hayo ya Afrika kwa niaba ya serikali ya Urusi.

Waziri wa Mambo ya nje wa Uingereza, David Lammy amesema vikwazo hivyo vitasaidia kuizuia Urusi kutikisa uthabiti wa mataifa ya Afrika na kuzuia uingizwaji wa silaha.

Le ministre britannique des Affaires étrangères, David Lammy, en fonction depuis le 5 juillet 2024. (Data archive) Il est membre du Parti travailliste.
Waziri wa Mambo ya nje wa Uingereza, David Lammy. © Reuters – Leon Neal / RFI archive

Hatua hii ya Uingereza ni vikwazo vya kwanza kuchukuliwa na taifa la G7 kulenga kampuni za ulinzi za Urusi, ambazo zinazshirikiana na mataifa kadhaa za Afrika kuzisaidia kwenye suala la ulinzi.

Vikwazo hivi vimekuja kuelekea mkutano mkubwa wa Mawaziri wa Mambo wa nje wa Mataifa ya Afrika uliotishwa na serikali ya Urusi, utakaofanyika mwishoni mwa wiki hii jijini Sochi kujadili ushirikiano wa masuala mbalimbali ya nchi hiyo na mataifa ya Afrika.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment