Afrika: Mataifa yalioathirika na Mpox yatengewa dozi laki 8 za chanjo

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Dozi zaidi ya laki 8 za awali za chanjo zimetengwa kwa ajili ya nchi 9 barani Afrika ambazo zimeathiriwa pakubwa na ongezeko la wagonjwa wa mpox, WHO na mashirika mengine ya afya yamesema.

Kulingana na takwimu za hivi karibuni, bara Afrika limerekodi wagonjwa wanaofikia elfu 46 wa Mpox, huku vifo vikivuka watu elfu moja.
Kulingana na takwimu za hivi karibuni, bara Afrika limerekodi wagonjwa wanaofikia elfu 46 wa Mpox, huku vifo vikivuka watu elfu moja. REUTERS – Stringer

Mwezi Septemba, baada ya kukabiliwa na ukosoaji kutokana na kasi ndogo ya ugavi wa chanjo hizo, WHO iliidhinisha chanjo ya majaribio ya kampuni ya Bavarian Nordic’s na kuahidi kuifanyia tathmini chanjo nyingine inayotengenezwa na kampuni ya dawa ya Japan, KM Biologic.

Aidha WHO ilianzisha mpango wa kusaidia kuleta chanjo ya mpox, vipimo na matibabu kwa watu walio hatarini zaidi katika nchi masikini duniani, juhudi sawa na zilizofanyika wakati wa janga la COVID-19.

Mataifa ya Afrika yalioathirika pakubwa na Mpox yanatarajiwa kuwa miongoni mwa yale yatakayopata chanjo ya mpox.
Mataifa ya Afrika yalioathirika pakubwa na Mpox yanatarajiwa kuwa miongoni mwa yale yatakayopata chanjo ya mpox. © François Lo Presti / AFP

Katika taarifa yake, shirika la afya duniani limesema, chanjo hizi mpya zitatolewa kwa nchi za Jamhuri ya Afrika ya Kati, Ivory Coast, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, KenyaLiberiaNigeriaRwandaAfrika Kusini na Uganda, huku zaidi ya asilimia 85 ya chanjo hizo zitatolewa kwa DRC iliyoathiriwa zaidi na ugonjwa wa Mpox.

Kulingana na takwimu za hivi karibuni, bara Afrika limerekodi wagonjwa wanaofikia elfu 46, huku vifo vikivuka watu elfu moja.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment