Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Kwa mara ya pili ndani ya miaka minane, mgombea mwanamke ameshindwa kwenye uchaguzi wa urais nchini Marekani.
Hali hii imejirudia kama ilivyokuwa mwaka 2016, wakati Hillary Clinton alipoweka historia ya kuwa mwanamke wa kwanza kuwania urais kupitia chama cha Democratic.
Mwaka 2024, Makamu wa rais Kamala Harris alijitosa ulingoni, kutafuta urais wa Mareani, baada ya rais Joe Biden kujiondoa, lakini amegonga mwamba.

Hillary Clinton na Kamala Harris wote wamepambana na Donald Trump kwa nyakati tofauti, ambapo suala la chuki dhidi ya wanawake, lilijitokeza wakati wa kampeni.
Trump alimwelezea Harris kama mwanamke asiyekuwa na akili timamu na asiye na uwezo wa kuongoza, suala ambalo wachambuzi wanasema huenda limechangia kutofanikiwa kwake.
Trump ameshinda uchaguzi huu licha ya madai ya unyanyasaj wa kimapenzi dhidi ya wanawake, madai ambayo ameendelea kukanusha.
Wakati wa kampeni wa mwaka 2024, Kamala ambaye aliandama na wanamuziki na watu mashuhuri kama Beyonce, Jennifer Lopez, Lady Gaga na Oprah Winfrey kuvutia wapiga kura wa kike, na kuwa katika mstari wa mbele kuahidi haki za wanawake, ikiwemo haki ya kutoa mimba, lakini ahadi hizo hazikutosha kumpa ushindi.
Chama cha Democratic mara mbili sasa, kimejaribu bila mafanikio kumwezesha mwanawake kuongoza Marekani swali ni nje, Wamarekani hawajawa tayari kuongozwa na mwanamke?
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.