Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Unataka KUONGEZA MAUZO Mara 2 Au Zaidi?…
Mbinu 6 Za Kuhakikisha Mteja Ananunua.
i. Onesha uharaka / dharura (The Urgency Close)
ii. Unampa orodha ya kuchagua (The Option Close
iii.Unafanya kama ameshakubali (Assumptive Close
iv. Unampa Mapendekezo (Suggestive Close)
v. Ondoa kitu kwenye ofa yako (Take away closes)
vi. Soft Closes
Katika Makala Hii Tutazungumzia Mbinu Ya Tano
– Ondoa Kitu Kwenye Ofa Yako (Take Away Closes)
Hapa kama mteja anasema kitu ni ghali sana…
…unaondoa baadhi ya bidhaa/kupunguza kitu fulani kisha unamshushia bei.
Wateja wengi ukiwafanyia hivi, kisaikolojia watakuwa hawataki kupoteza ulichopunguza.
Na wanaanza kuona ulichokitoa ni cha muhimu sana.
Ndio maana unataka kubaki nacho, mwishoni wataamua kununua tu.
Mfano: Unauza simu, unamwambia hii simu iko na full package:
Ina charger, battery moja ya ziada na earphone.
Una mwambia kuwa ukimpa vitu vyote unamuuzia 150,000/=.
Kama mteja atasema bei hiyo ni ghali na anasema kuwa anataka umuuzie kwa 100,000/=.
Unachofanya kama muuzaji, haumkatalii.
Bali unamwambia kuwa, kwa bei hiyo nitakuuzia simu…
…ila nitabakia na betri ya ziada na charger pia hautapata.
Kisaikolojia imeonekana kwamba, wateja wengi sana wakiona unaondoa kitu baada ya kuomba kupunguziwa bei…
…huwa wanaamini unachotoa ni cha thamani sana na pia wanaumia kupoteza.
Kwa sababu ya aina hiyo ya maumivu huwa wanaamua kupanda bei ili wakipate.
Na hapo itakusaidia kuwauzia kwa bei nzuri zaidi yenye faida upande wako.
Ukifanya hivi hata kama hawatafika kwenye bei ya awali uliyowatajia…
…ila watakuwa tayari kuongeza tena kidogo ili wapate vyote.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.