Israeli imeiandikia UN kuhusu hatua yake ya kusitisha makubaliano na UNRWA

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Israel imethibitisha kutoa taarifa kwa Umoja wa Mataifa kuhusiana na hatua yake ya kusitisha ushirikiano wake na UNRWA, shirika linalotoa misaada kwa raia wa Palestine.

Israeli inasema wafanyikazi wa UNRWA, walishiriki katika shambulio la tarehe 7 ya mwezi Oktoba na kwamba wafanyikazi wake wengi ni washirika wa Hamas.
Israeli inasema wafanyikazi wa UNRWA, walishiriki katika shambulio la tarehe 7 ya mwezi Oktoba na kwamba wafanyikazi wake wengi ni washirika wa Hamas. © Amr Abdallah Dalsh / Reuters

Hatua ya Israeli imekuja baada wabunge kupiga kura kupiga marufuku shughuli za shirika hilo.

Katika taarifa yake, Wizara ya mambo ya kigeni ya Israeli imesema imetekeleza maagizo ya Israel Katz, Waziri wa mambo ya nje wa Israeli ya kukatisha makubaliano kati yake na shirika la UNRWA.

Israeli inasema wafanyikazi wa UNRWA, walishiriki katika shambulio la tarehe 7 ya mwezi Oktoba na kwamba wafanyikazi wake wengi ni washirika wa Hamas.

Hatua ya Israeli imekuja baada wabunge kupiga kura kupiga marufuku shughuli za shirika hilo.
Hatua ya Israeli imekuja baada wabunge kupiga kura kupiga marufuku shughuli za shirika hilo. © Ariel Schalit / AP

Aidha Israeli imeeleza kwamba shirika hilo ni sehemu ya matatizo yanyoshuhudiwa katika Ukanda wa Gaza na kwamba halitoi suluhu ya mzozo.

Bunge la Israeli mwezi uliopita liliidhinisha mapendekezo ya kusitisha shuguli za UNRWA katika maeneo yanayodhibitiwa na Israeli na kaskazini mwa mji wa Jerusalem,licha ya hatua hiyo kupingwa na jamii ya kimataifa na Marekani.

Wachambuzi wa mambo ya kimataifa wanasema hatua ya Israeli kulipiga marufuku kundi hilo itakuwa pigo kwa juhudi za utoaji wa misaada ya kibinadamu katika ukanda wa Gaza.

Israeli inawatuhumu wafanyikazi wa UNRWA kwa kuhusika na shambulio la Hamas na mwaka uliopita.
Israeli inawatuhumu wafanyikazi wa UNRWA kwa kuhusika na shambulio la Hamas na mwaka uliopita. AFP – EYAD BABA

Waziri wa mambo ya kigeni wa Israeli Katz kwa upende wake ametupilia mbali hofu kwamba hatua ya nchi yake italeta changamoto kubwa kwa raia wa Gaza na kwamba sehemu ndogo ya misaada ilikuwa inafikishwa katika ukanda huo na UNRWA.

Mwezi Januari, Israel iliwatuhumu wafanyikazi wa UNRWA katika ukanda wa Gaza kwa kuhusika na shambulio la Oktoba 7 mwaka wa 2023 ambalo lilioongozwa na Hamas.  Inahofiwa kuwa hatua ya Israeli pia huenda ikatoa changamoto kwa wafanyikazi wa UNRWA kutembea kutoka sehemu moja hadi nyengine kutokana na vizuizi vya Israeli.

UNRWA na mashirika mengine ya kutoa misaada yameituhumu Israeli kwa kuzuia usambazaji wa misaada katika ukanda wa Gaza ambapo zaidi ya watu Milioni 2.4 wamepoteza makazi yao kutokana na mapigano yanayoendelea.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment